Mkandarasi anawajibika kutekeleza mradi aliyopewa kwa kiwango kinachokubalika na baadaye hukaguliwa na kama mradi umekidhi kiwango basi anatakiwa kulipwa haki yake. Kwa siku za karibuni mambo siyo rafiki sana kuhusu malipo ya Wakandarasi hasa TARURA.. Mkandarasi unamaliza kazi na hatua zote zimepitiwa mpaka ukaguzi halafu unaambiwa kuwa usubiri malipo. Ikumbukwe kuwa Serikali kwa makusudi mazima iliongeza tozo ili barabara za vijijini ziweze kutengenezwa lakini mbona hali ya malipo siyo kama ilivyoahidiwa?. Naona hapa kasoro hizi siyo za TARURA ila ni za Serikali. Inavyoonekana TARURA Makao makuu hawapewi fedha na Serikali kwa wakati ndiyo maana mambo kama haya yanatokea. Ninashauri mkandarasi anapomaliza kazi yake basi alipwe mara moja.