Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Kukosekana au kufungwa kwa Duka hiilo lililopo ndani ya Hospitali ya Manispaa ya Mpanda katika makao makuu ya Mkoa ni jambo ambalo halipendezi na limetuacha katika maswali mengi.
Baada ya duka hilo kuwakuwa linafanya kazi, sasa Wagonjwa na Wananchi wengi wenye uhitaji tunalazimika kwenda kwenye maduka ya Watu Binafsi yaliyopo nje ya Hospitali kwenda kununua huko.
Natoa wito kwa Serikali hasa kwa mamlaka husika na huduma hiyo, warejeshe kwa Duka la MSD kwani ni tegemeo kwetu na msaada mkubwa hususani kwa Wananchi ambao hushindwa kumudu gharama za bei za maduka binafsi ya dawa.