Kulikoni Ruby kakumbwa na nini?

Kulikoni Ruby kakumbwa na nini?

Nimesikiliza East Africa Breakfast ya jumapili Leo, East Africa Radio mtangazaji anamwonya Ruby bado tunakupenda na tunakuhitaji, anamalizia kwa kusema chondechonde. Hakutaka kuweka mambo hadharani Redioni.

Je Ruby kakumbwa na nini jamani?
Ruge!!!!!!
 
Mkuu fundi bishoo tatizo la taifa hili ndio hilo kaka, kitu kidogo tu siasa. Sasa wewe Radio inasikilizwa na watu wa rika zote na unamzungumzia msanii kwa nini usiweke wazi badala ya kupiga blah blah unaongea kwa mafumbo ili iweje? kama umeamua kuongea ukweli ongea tu ama laa basi nyamaza? Halafu wanakuja watu wanawapa rank hawa watangazaji uchwara.
Na angefanya hivyo kwa kusema wazi nisingekuja na huu Uzi humu. Kanikera kweli!
 
Sasa na mwili ule akiwa anakula ngada si ndio atabaki mifupa? Ila madada wanaingia kwenye madawa ya kulevya kwa kudanganyana kwamba inakupa english figa na vijana wa kiume wanajidanganya kwamba ukipiga bwimbwi unasimamia shoo za kibabe ila matokeo yake wanakuwa MATEJA.
 
Hivi inakuaje haya madawa unawaona kabisa wenzako wakipukutika alafu na wewe unaenda kujaribu?
Ni kama ilivyo Ngono, unaona kabisa watu wanakata kamba kwa UKIMWI, lakini stills watu wanapiga nyabe mtelezo!

Huu ni ugonjwa kama ugonjea mwingine tu!....Rubby asaidiwe!
 
"Maisha ni mchanganyiko wa taabu nyingi sana,zilizo ambatana na chembe chembe ndogo sana za raha ambazo hazikawii kuyeyuka".

Mwamuzi wa Maisha yako ni wewe Mwenyewe.

Also,Happiness is a choice.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom