Kulikoni Tendwa na Jeshi la polisi?

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
3,768
Reaction score
4,038
Nilikuwa nasikiliza vyombo vya habari, nikamsikia msajili wa vyama vya siasa mzee Tendwa akiwaambia askari polisi kuwa wawachukulie hatua za kisheria viongozi wa vyama vya siasa watakaosababisha vurugu kwenye chaguzi zinazokuja.

Wana JF nisaidieni, Mimi ninavyo fahamu CCM ndo inasababisha vurugu za kisiasa kwenye chaguzi, je askari wataweza kupambana na CCM kweli kama wanavyopambana na vyama vingine?
 
Mwaka huu tutaona na husihia mengi. Kichaa kakabidhiwa rungu aingie sokoni. Tusubiri matokeo
 
Maana sehemu nyingi ccm/serikali ndo wanaanzisha fujo kwa kupeleka askari sehemu ambazo wasingepaswa kuwepo, je hawa askari wataweza kupambana na ccm/serikali iliyowatuma?
 
Nimesoma gazeti moja leo huyo huyo tendwa mwenyewe anakiri kuwa naye anahusika na vurugu za uandikishaji huko Pemba na Unguja. basi hao polisi waanze kumchukulia yeye hatua
 
Nimesoma gazeti moja leo huyo huyo tendwa mwenyewe anakiri kuwa naye anahusika na vurugu za uandikishaji huko Pemba na Unguja. basi hao polisi waanze kumchukulia yeye hatua

Mwe!!!!!!!!!!.
Kama ndivyo ilivyo, basi tusubiri. Kama polisi hatamchukulia hatua, basi watakuwa ni pandikizi tu la ccmna si vinginevyo.
 
Wana JF nisaidieni, Mimi ninavyo fahamu CCM ndo inasababisha vurugu za kisiasa kwenye chaguzi, je askari wataweza kupambana na CCM kweli kama wanavyopambana na vyama vingine?
Kuweza kupata majibu mazuri ya hoja tusianze kuwa biased, Tendwa akasema viongozi wa vyama vya siasa, kama CCM ni chama cha siasa basi wakifanya vurugu wanapaswa kushughurikiwa, sioni kama amekosea hapa.
 
Kwa tafsiri ya polisi, vyama vya siasa ni vyama vya upinzani. CCM ni chama tawala na ndiyo chenye dola. "Mbwa wako mwenyewe akianza kukung'ata basi unamwachilia mbali kama Rais wa zamani wa Ufaransa Chirac alivyofanya baada ya mbwa kuwa anamg'ata baada ya kukosa zile huduma kama alizokuwa anapata ikulu".
 
Kuweza kupata majibu mazuri ya hoja tusianze kuwa biased, Tendwa akasema viongozi wa vyama vya siasa, kama CCM ni chama cha siasa basi wakifanya vurugu wanapaswa kushughurikiwa, sioni kama amekosea hapa.

Kufikiria tu kuwa CCM wanaweza kushughulikiwa ni kuwa biased, haijatokea, haitokei na haitatokea so long as CCM iko madarakani. Jeshi letu la polisi ni la kisiasa zaidi. Lini ulisikia CCM inashughulikiwa???? Pamoja na watu kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…