Kulikoni Vodacom Mpesa Mastercard?

Kulikoni Vodacom Mpesa Mastercard?

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Katika hali ya kushangaza leo niliomba kuangalia mini statement kwenye akaunti zangu za Vodacom.

Nimebaini kuwa pesa zangu zilizokuwa kwenye akaunti ya Mastercard zimerudishwa Mpesa.

Hivi sasa huduma ya Mpesa Mastercard imeondolewa kabisa kwenye menu.

Inawezekana Vodacom walitangaza mabadiliko hayo mimi sikusikia, kupitia jukwaa hili nawaomba Vodacom watoe ufafanuzi juu ya kusitishwa kwa huduma hii kwani ilikuwa inatusaidia kwenye manunuzi mtandaoni. Naomba kuwasilisha.
 
Wamebadlisha kwenda visa card na unatakiwa ufungue account upya , huenda mkataba wao na bank ABC umeingia shubiri
Wamebadilisha kimya kimya bila hata kutoa maelezo?. Ile ilikuwa Virtual Mastercard na kwenye menu yao ilikuwepo pamoja na Mpawa, Sasa hivi hata hiyo Virtual Visa Card haipo.
 
Walituma ujumbe
 
1- Kwanza walituma message kama una pesa Mastercard hamisha.

2- Baadaye wakatuma tena SMS hawatumii tena Mastercard.

3- Baadaye wakatuma sasa hivi wanatumia M-pesa Visa Card
 
1- Kwanza walituma message kama una pesa Mastercard

Ok. Nashukuru kwa maelekezo,lakini nashangaa hata kwenye menu haipo? Labda inatolewa na Bank of Africa? au ABC Bank iliyotajwa na mdau humu?.
 
1- Kwanza walituma message kama una pesa Mastercard

2- Baadaye wakatuma tena SMS hawatumii tena Mastercard.

3- Baadaye wakatuma sasa hivi wanatumia M-pesa Visa Card
Hii ipo kwenye menu yao? Jana nilikuwa na shida sikuona hiyo kitu.
Nafikiria kwenda kupata card bank tu.
 
W
Wamebadilisha kimya kimya bila hata kutoa maelezo?. Ile ilikuwa Virtual Mastercard na kwenye menu yao ilikuwepo pamoja na Mpawa, Sasa hivi hata hiyo Virtual Visa Card haipo.
Walitoa taarifa na walipomaliza wakatoa tena taarifa.
 
Hii ipo kwenye menu yao? Jana nilikuwa na shida sikuona hiyo kitu.
Nafikiria kwenda kupata card bank tu.

Naomba ulizs hivi voda visa( awali mastercard) inaweza ku accept deposit kutoka kwa third part bila wewe kuiload money?
 
Wamebadilisha kwenda visa card, walitoa taarifa, wakaturudishia pesa zetu.

Pia kufungua card mpya ya visa na rahisi kama ilivyokuwa Mastercard.
 
Back
Top Bottom