Kwa kuangalia ukweli na jinsi manispaa zinavyojiendesha hivi vitambulisho vimewaumiza sana manispaa zote nchini.
kwa siku mfano hapo Segerea ushuru wa soko,mama ntilie nk ulikuwa ni kama laki 3 hivi.so kwa mwezi ni 300000x30 ni milion 9.hapo ni stand tu.b Bdo sehem zingine.
vitambulisho vya machinga kwa siku 360 ni tzs 20000. na hii hela inaenda ofisi ya rais. je manispaa inafaidika na nini kwa uwepo wa wa fanya biashara wadogo kwenye maeneo yake ambapo kila baada ya saa 24 manispaa zinatakiwa kuondoa uchafu uliozalishwa na hava wafanya biashara? Kuhakikisha ulinzi(mgambo) wapo wa kutosha nk.
Serikali kwa hili inatakiwa ijitafakari na kuja na suluhisho la kudumu. Pale Kariakooo zaidi ya million tano zinapotea kila siku kuingia kwenye mapato ya wilaya ya ilala,lakini itokee siku Kariakoo apajasafishwa, taka zake zitajaza malori zaidi ya 50 nani analipia huu usafi na kwa hela toka mfuko upi?
Kwa sasa viongozi wengi wana fanya kazi na kutimiza majukumu yao katika mazingira magumu na yenye bajeti kiduchu au zero kabisa.