Kulima Mahindi kumekuwa tatizo

Vivax

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
520
Reaction score
184
Wakulima wa Mahindi wanahaha hawajui cha kufanya. Wanavuna miezi hii lakini bei ni mbaya sana kulingana gharama za uzalishaji.

Kwa wakulima wa pale Mbeya Farm price ni sh 150/=kwa kilo au kwa kipimo wanachokiamini Wao (plastic ya 20 litres) ni she 3000/= shambani kwake
 
Ni muda muafaka kwa wakulima kuungana na kuangalia njia mbadala za kuongeza thamani ya zao husika (add value) wakati wa mavuno. Sio lazima wauze mahindi. Wanaweza kusaga na kuuza unga au kukoboa na kuyauza kama kiungo cha Makande. Watanzania tuache kulialia.
 
Waanzishe vijiwe vya mahindi ya kuchoma na kumchesha huku Dar, muhindi choma mmoja laini na ulioiva vizuri unauza hadi 500/=, sasa kwanini usubiri kusaga unga na kuuza kilo buku?
 
Hili la mahindi nalo limekuwa tatizo sasa
 
Nasikia bei ya Mahindi huko Sumbawanga ni 15,000 mpaka 18,000 kwa gunia.
 
According to your comment, hujui unachoongea value addition kwenye mahindi ni kitu kingne kabisa wala sio kuuza unga kama unavyofikiria.
 
Sumbawanga mahindi hakuna. Katafute uone kama utapata. Mavuno mabaya ...usishangae ukiona bei imefika laki mwaka huu...unless serikari yenu iamuwe kuwakandamiza wakulima tena kwa kufunga mipaka...lakini hapa sumbawanga tunapeleka congo gunia sh. 80,000.
 
Waanzishe vijiwe vya mahindi ya kuchoma na kumchesha huku Dar, muhindi choma mmoja laini na ulioiva vizuri unauza hadi 500/=, sasa kwanini usubiri kusaga unga na kuuza kilo buku?


Hatari hii, yaani huu ndio ushauri wako kwa mkulima wa mahindi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…