Kumbe aliyekuwa anaogopewa ni hayati Magufuli lakini siyo utawala wake, Magufuli Bus Terminal mambo ni vurugu tupu!

Kumbe aliyekuwa anaogopewa ni hayati Magufuli lakini siyo utawala wake, Magufuli Bus Terminal mambo ni vurugu tupu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli hayati Magufuli aliogopwa yeye binafsi na wala siyo utawala wake kwa sababu kuna maeneo mambo ni vurugu tupu lakini watendaji ni wale wale.

Nimefika Magufuli Bus Terminal utaratibu wa ukataji tiketi na mpangilio wa mabasi ni hovyo kabisa.

Kwenye parking ya mabasi yaani wanapaki hadi barabarani na kuzibiana njia, basi la kuondoka saa 12 asubuhi linaweza kuondoka saa 1:15 kwa sababu tu ya kuzibiwa njia na mabasi mengine.

Mkuu wa mkoa liangalie hili.

Pili kwa sababu parking ina uwezo wa kuchukua mabasi 108 na mabasi yanayotoka asubuhi ni zaidi ya 200 basi yaruhusuni mabasi yanayoanzia Shekilango yasiingie hapo stendi kuu Mbezi.

Eid Mubarak!
 
Watendaji timizeni wajibu wenu, msiwe watu mnaohitaji kupigiwa kelele kila siku eti tu kwasababu flani alikuwa mkali hayupo na nyie mnalala. Na jambo kama hili halihitaji hata Rais, kwani mkuu wa mkoa, wakurugenzi na mamlaka nyingine husika wanafanya kazi gani?
 
Hivi kweli serikali Ijenge stand ya mabasi halafu Rais aje asimamie mipangilio ya mabasi kweli, halafu mtu unakuja kumlaumu mwendazake hii ni akili matope. Sema ustaarabu hatuna full stop. Tumepewa kitu kizuri tuwe wastaarabu.
 
Watendaji timizeni wajibu wenu,msiwe watu mnaohitaji kupigiwa kelele kila siku eti tu kwasababu flani alikuwa mkali hayupo na nyie mnalala.Na jambo kama hili halihitaji hata Raisi, kwani mkuu wa mkoa,wakurugenzi na mamlaka nyingine husika wanafanya kazi gani?
Yaani watendaji wamejisahau mno!
 
Bi Samia ana kibarua kigumu mbele yake, inaweza kuchukua karibia miezi 18 kuweza kurudisha Utawala wenye kufuata Sheria na taratibu za Nchi, Magufuli alifanya kazi yeye kama yeye na hakuzingatia maisha ya raia wengine kwa kupuuza au kuzifutilia mbali taratibu za mipango miji.
 
Hivi kweli serikali Ijenge stand ya mabasi halafu Rais aje asimamie mipangilio ya mabasi kweli , halafu mtu unakuja kumlaumu mwendazake hii ni akili matope . Sema ustaarabu hatuna full stop. Tumepewa kitu kizuri tuwe wastaarabu.
Mimi nashangaa watu wanapenda kurudia kusema hii kauli ya "kuweka system" hawajui kuwa watu bila kujijengea utamaduni mzuri hata hizo system hazitofanya kazi, watu wenyewe hawana ustaarabu kama unavyosema wanataka kuongozwa kama mifugo.
 
Watendaji timizeni wajibu wenu,msiwe watu mnaohitaji kupigiwa kelele kila siku eti tu kwasababu flani alikuwa mkali hayupo na nyie mnalala. Na jambo kama hili halihitaji hata Raisi, kwani mkuu wa mkoa,wakurugenzi na mamlaka nyingine husika wanafanya kazi gani?
Kwani Wazungu waliposema watoto wasipigwe bakora shuleni walikuwa wajinga? Walijuwa kuwa binadamu unatakiwa uwajengee system iliyo rahisi kuifata ili iwe endelevu. Walijuwa kuwa kuna Wanafunzi wataonekana wanafanya vizuri kumbe sababu ya kuogopa bakora. Lakini uhalisia ni kuwa akiwa nje ya shule hakutokuwepo mtu wa kumpiga bakora. Na kwa vile alionekana anafanya uzuri shule angeweza kupewa uongozi baada ya shule na kumbe hamna kitu kichwani.

My point is, uongozi sio vitisho. Chagua watu kutokana na uwezo wao wa kuweza kujiendesha wenyewe na kuwaongoza wenziwao. Kama mtu hawezi kujiongoza mpaka akaguliwe na kutukanwa kila siku basi huyo hafai!
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Wanadamu na ubinafsi, ili uwabadlishe lazima uwe mwamba kwelikweli

Sasa hivi huko Nyerere atakua anamwambia hata yeye alisalitiwa hivyo hivyo kwenye falsafa ya ujamaa

Gadafi nae anamkumbusha vile yeye alifanya mema sana kwa watu wake tena kwa miaka mingi lakini walimuua

Endelea kupumzika kwa amani kipenzi chetu John Pombe Magufuli, Mwamba, Shujaa na rais wa karne

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
 
Back
Top Bottom