Dong Jin
JF-Expert Member
- Jun 4, 2018
- 968
- 2,034
Mwanzoni mwa utawala wa mama Samia, kuna mkopo wa trilioni 1.3 wa masharti nafuu ambao ulikopwa kwa ajili ya kupambana na janga la korona.
Huu mkopo ulipata umaarufu zaidi baada ya aliyekuwa spika wa bunge mh. Job ndungai kuhoji kwanini mkopo huo umeombwa wakati tunaweza kutumia hela zetu za makusanyo ya ndani? Tokea hapo drama za huu mkopo zikaanza.
Kila wizara ilijinadi kupewa kiasi fulani kufanya maendeleo makubwa na mbalimbali katika nchi yetu. Wizara ya afya walipewa zaidi ya bilioni 400, wizara ya elimu bilioni 300+, hivohivo kwa wizara ya maji, wizara ya kilimo, wizara ya ujenzi, tamisemi, na kadhalika!
Sasa kama trilioni 1.3 imeweza kufanya mambo makubwa namna hiyo, je trilioni 2 haiwezi kututosha kwa bajeti ya nchi?
Bajeti ya mh Mwigulu Nchemba imezidi hii ya covid. Sasa ni kwanini miradi mingi inahusiswa na hela za uviko? Au tulidanganywa kiasi sahihi kilichokopwa?
Mapambio ya huu mkopo yamekuwa mengi sana kuliko uhalisia wake. Tungeomba yaendane na uhalisia maana tunadanganywa sana chini ya kivuli cha huu mkopo!
Nawasilisha