Kumbe Bangi ina aina zaidi ya 100 na ladha tofauti

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Nilikuwa sijui kama bangi ina ladha tofauti tofauti, sasa jana kuna muuzaji mmoja wa Bangi huko Marekani kanipa kazi ya kumwandikia review za species 100 za bangi ambazo alinipa majina yake, ili aweze kuuza Amazon na kwingineko.

Hivyo nikaingia chimbo kabla ya kuanza kuandika hiyo review.
Nikashangaa, kwanza zimegawanya katika indica, kuna hybrid halafu kuna sativa
Halafu zinazalishwa kwa cross breeding.

Kuna bangi mfano 9 lb Hammer, ina ladha ya mchanganyiko wa zabibu, limao, apple, na udogo pamoja na sukari.

Kuna nyingine ina ladha ya apple cider, na nanasi
Na kila moja inafaida yake.

Kuna inayotibu matatizo ya usingizi kama insomnia, pamoja na depression.
Nyingine inatibu matatizo ya misuri na hasira.
Tahadhari msivute bangi siyo jambo zuri kutokana na sheria ya Tanzania...
 
Ulivyoilezea vizuri, nimetamani niionje kidogo hasa hiyo yenye ladha ya apple na zabibu. Itakuwa ndo anayotumia yule jamaa wa kumpiga mateke Mbasha.
 
Hizo ni rizla fleva tu;

Ganja inapimwa kwa eneo inapolimwa Mfano sehemu za baridi, bondeni, mlimani nk.

Aidha hutegemea pia uchumaji na I chambuaji wake. Ganja ikichumwa ikiwa haijakomaa huwa tofauti na ile iliyokomaa (katika stimu)

Pia ganja nzuri huwa ile yenye nta ambayo ukiivuta rizla inaloana mafuta wenyewe wanaita nta.

Bangi mbaya ni ile ya mapushabu yaani imechambuliwa na Yale yaliyobaki mtu anaamua kunyonga na kuvuta.

Ile ya Adam itakua ni bangi ya Arusha ambayo alivuta mchana akaipandisha na Fegi Portsman [emoji23]
 
Hii 9 lb Hammer ndio ninayo itumia kama mboga...[emoji41][emoji41]
 
Sasa hizi yani zinatofautiana mmea na mmea kuanzia majani taste, aroma, effects -/+ na species na element percentage na zinafanyiwa cross bleeding mfano hiyo 9 lb Hammer ilitengeneza Jinxproof Genetics ni kampuni ya mambo ya kutengeneza mbegu hizi za GMO
 
Nakushauri wahi mirembe labda utaweza kuokoa akili kidogo ulizobakiwa nazo kichwani maana kwa kiasi kikubwa 'medula' imeshaharibika!
 
Hahaha haya makitu sio kabisa, enzi hizo pale University of Denver kwa nyuma tu kabla hujafika Colorado BLVD barabarani kuna dent mmoja kwa ushabiki alikwenda dispensary moja hapo, akavuta ma flavor tofauti, mpaka leo kiziwi.

Anatumia hearing aid alifukuta moshi alipotoka pale akawa hasikii mpaka akatibiwa masikio lakini wapi, akapewa hearing aid.

Kila nilikuwa nikimuangalia nakumbuka alivyokuwa na leo alivyo nabaki kucheka tu.

Haya mavitu hata sijui huwa yana shida gani, kuna watu hawaathiriki na kuna watu huathirika vibaya.

Nadhani flavor ni nyingi sana.

Sio kila kitu kina jaribiwa, kuna vingine unaviacha huko huko kwenye story.
 
Usicheze na bangi ya msumgiji. Hii ya Arusha hata kuku anaweza kuila ukimtilia kwenye maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…