Kumbe bila mpinzani mwanamke hajali

Kumbe bila mpinzani mwanamke hajali

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Siku za hivi karibuni mke wangu amekuwa akionyesha tabia za kutojali,mfano,unaweza ukawa kazini ukamtext," hi baby" akajibu "P"
Ukiendelea anapiga kimya hajibu sms,.

Kwa kuwa muda wake wa kutoka kazini kwake yeye huwa ni SAA 9,mimi huwa ni SAA 11 jioni,nikifika nyumbani ile hali ya kunipokea hana,na nikimsalimia anajibu kama hataki vile.
Tukiwa tumelala,yeye husogea pembeni mwa kitanda,nikimsogelea hataki nimshike
Nimejaribu kumuuliza tatizo ni nini yeye hujibu tu" hamna kitu" yupo kawaida,
Karibia mwezi mmoja sasa tabia hii ikawa inaendelea,lakini huko nyuma hakuwa hivyo,alikuwa anaajibika kama mke, alikuwa anajua wajibu wake kwangu lakini amebadilika sana kwa sasa

Ili nibaini tatizo ni nini kinamsumbua nilimtuma shoga ake amuulize nimemkosea nini,majibu yaliyotoka kuwa ana stress tu,nikajaribu kumuuliza niambie stress za nini hakutaka kuniambia

Nikawaza,nikawazua ,maana furaha ya ndoa siioni tena.
Hapa mtaani kuna mdada ni rafiki yake huyo shoga yake mke wangu,nikaanza kumtongoza tena nikiwa serious, na nikafanya makusudi ili mke wangu apate hizo habari, yule Dada akamwambia rafiki yake huyo ambaye ni rafiki wa mke wangu,
Mke wangu akapata taarifa juu ya struggle zangu kwa huyo mwanadada.Ghafla nimeanza kuona mabadiliko kutoka kwa mke wangu,sasa hivi yeye ndo ananitumia SMS kila nusu saa,baby,dear,love kibao,nikirudi nyumbani mapokezi ya nguvu,tukilala nasogelewa ile mbaya,baba fulani zimekuwa nyingi siku hizi

Mpaka na mimi nimeshangaa kwa haya mabadiliko,na cha ajabu zimepita wiki mbili hajaniuliza kuhusu kumtongoza huyo Dada,

Wanawake bwana sijui wameumbwaje,bila mpinzani hamuendi kabisa
 
Wapo wanaozidisha upendo wawapo bila upinzani.

Lakini walio wengi bila upinzani hawajali wala kukupa priority.
Wengine hujisahau na kubweteka kabisaa.
 
Yap huwa wanajisahau.. hawajali tena. Mpaka watakapoanza kupata fununu kuwa nafasi yake imepata upinzani. Ndipo hapo huanza kurudisha majeshi.
 
Siku za hivi karibuni mke wangu amekuwa akionyesha tabia za kutojali,mfano,unaweza ukawa kazini ukamtext," hi baby" akajibu "P"
Ukiendelea anapiga kimya hajibu sms,.

Kwa kuwa muda wake wa kutoka kazini kwake yeye huwa ni SAA 9,mimi huwa ni SAA 11 jioni,nikifika nyumbani ile hali ya kunipokea hana,na nikimsalimia anajibu kama hataki vile.
Tukiwa tumelala,yeye husogea pembeni mwa kitanda,nikimsogelea hataki nimshike
Nimejaribu kumuuliza tatizo ni nini yeye hujibu tu" hamna kitu" yupo kawaida,
Karibia mwezi mmoja sasa tabia hii ikawa inaendelea,lakini huko nyuma hakuwa hivyo,alikuwa anaajibika kama mke, alikuwa anajua wajibu wake kwangu lakini amebadilika sana kwa sasa

Ili nibaini tatizo ni nini kinamsumbua nilimtuma shoga ake amuulize nimemkosea nini,majibu yaliyotoka kuwa ana stress tu,nikajaribu kumuuliza niambie stress za nini hakutaka kuniambia

Nikawaza,nikawazua ,maana furaha ya ndoa siioni tena.
Hapa mtaani kuna mdada ni rafiki yake huyo shoga yake mke wangu,nikaanza kumtongoza tena nikiwa serious, na nikafanya makusudi ili mke wangu apate hizo habari, yule Dada akamwambia rafiki yake huyo ambaye ni rafiki wa mke wangu,
Mke wangu akapata taarifa juu ya struggle zangu kwa huyo mwanadada.Ghafla nimeanza kuona mabadiliko kutoka kwa mke wangu,sasa hivi yeye ndo ananitumia SMS kila nusu saa,baby,dear,love kibao,nikirudi nyumbani mapokezi ya nguvu,tukilala nasogelewa ile mbaya,baba fulani zimekuwa nyingi siku hizi

Mpaka na mimi nimeshangaa kwa haya mabadiliko,na cha ajabu zimepita wiki mbili hajaniuliza kuhusu kumtongoza huyo Dada,

Wanawake bwana sijui wameumbwaje,bila mpinzani hamuendi kabisa
Hii kitu si kwa mke tu hata girlfriends. Wanakuwa na hiko kitabia mkishakaa kwenye mahusiano kwa muda. Anazoea anakuwa hakujali tena, anakuwa mtu wa kukuchukulia powa. Kimbembe ni pale na ww unapoacha kujali ... na kumchukulia powa.. au akapata fununu kuwa umepata mwingine.

Wanashtuka na kutudi katika hali zao.. mapenz yanaongezeka na kuwa mengi.

Wito kwa wakina dada msisahau nafasi zenu mkidhani kuwa mwanaume ni mjinga. Kumbukeni kuwa wanawake ndio wengi kuliko wanaume, unapomsusia mumeo , au kumnunia bila sababu yotote.. unadhani unamkomoa au inabomoa ndoa na mahusiano yako? Badilikeni
 
Kipindi anakuchunia wewe alikua ananyenyekea kwingine...

Baada ya kugundua utaanza kunyenyekea kwingine, nae ndiyo anajirudi...

Cc: mahondaw
 
Vodacom premier league ilianza kunoga baada ya azam kuleta upinzan kwa simba na yanga
 
Hii kitu si kwa mke tu hata girlfriends. Wanakuwa na hiko kitabia mkishakaa kwenye mahusiano kwa muda. Anazoea anakuwa hakujali tena, anakuwa mtu wa kukuchukulia powa. Kimbembe ni pale na ww unapoacha kujali ... na kumchukulia powa.. au akapata fununu kuwa umepata mwingine.

Wanashtuka na kutudi katika hali zao.. mapenz yanaongezeka na kuwa mengi.

Wito kwa wakina dada msisahau nafasi zenu mkidhani kuwa mwanaume ni mjinga. Kumbukeni kuwa wanawake ndio wengi kuliko wanaume, unapomsusia mumeo , au kumnunia bila sababu yotote.. unadhani unamkomoa au inabomoa ndoa na mahusiano yako? Badilikeni
Nakuunga Mkono,hawalijui hilo
 
Mpaka mpinzani tena... mwanadada anapata mtu mpaka haamini macho yake anakulindaa kama yai acheni tuu
 
Duuh inawezekana nayeye alikuwa anatongozwa so alianzakuwaza nn afanye na aliyekuwa anamtongoza alianzakumwingia taratibu ndo maana akaanza kukupotezea,fuatilia vzr kazini kwake
 
Back
Top Bottom