Ketoka
JF-Expert Member
- Sep 23, 2015
- 1,117
- 1,966
Siku za hivi karibuni mke wangu amekuwa akionyesha tabia za kutojali,mfano,unaweza ukawa kazini ukamtext," hi baby" akajibu "P"
Ukiendelea anapiga kimya hajibu sms,.
Kwa kuwa muda wake wa kutoka kazini kwake yeye huwa ni SAA 9,mimi huwa ni SAA 11 jioni,nikifika nyumbani ile hali ya kunipokea hana,na nikimsalimia anajibu kama hataki vile.
Tukiwa tumelala,yeye husogea pembeni mwa kitanda,nikimsogelea hataki nimshike
Nimejaribu kumuuliza tatizo ni nini yeye hujibu tu" hamna kitu" yupo kawaida,
Karibia mwezi mmoja sasa tabia hii ikawa inaendelea,lakini huko nyuma hakuwa hivyo,alikuwa anaajibika kama mke, alikuwa anajua wajibu wake kwangu lakini amebadilika sana kwa sasa
Ili nibaini tatizo ni nini kinamsumbua nilimtuma shoga ake amuulize nimemkosea nini,majibu yaliyotoka kuwa ana stress tu,nikajaribu kumuuliza niambie stress za nini hakutaka kuniambia
Nikawaza,nikawazua ,maana furaha ya ndoa siioni tena.
Hapa mtaani kuna mdada ni rafiki yake huyo shoga yake mke wangu,nikaanza kumtongoza tena nikiwa serious, na nikafanya makusudi ili mke wangu apate hizo habari, yule Dada akamwambia rafiki yake huyo ambaye ni rafiki wa mke wangu,
Mke wangu akapata taarifa juu ya struggle zangu kwa huyo mwanadada.Ghafla nimeanza kuona mabadiliko kutoka kwa mke wangu,sasa hivi yeye ndo ananitumia SMS kila nusu saa,baby,dear,love kibao,nikirudi nyumbani mapokezi ya nguvu,tukilala nasogelewa ile mbaya,baba fulani zimekuwa nyingi siku hizi
Mpaka na mimi nimeshangaa kwa haya mabadiliko,na cha ajabu zimepita wiki mbili hajaniuliza kuhusu kumtongoza huyo Dada,
Wanawake bwana sijui wameumbwaje,bila mpinzani hamuendi kabisa