Mtanzania Tajiri
JF-Expert Member
- Aug 31, 2024
- 341
- 319
Tofauti sana na Watanzania wengi wanavyofikiria kuwa Hayati Mwl JK. Nyerere hakuihitaji Sekta binafsi PPP, Haya mawazo si ya kweli,
Ukweli wa wazi MwL JK. Nyerere aliamini zaidi kwenye Sekta binafsi kuwa ni ndio msingi pekee wa kuchochea na kuleta mitaji, Ujuzi na Teknolojia na zaidi sana kuchochea ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Serikali yake.
Leo, jambo j ema ni kuwa chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi wake David Kafulila ikiwa ni zaidi ya miaka sitini ( 60 ) imepita hatimaye mawazo ya Mzee huyu yanaingia kwenye utekelezwaji rasmi, Lazima Rais Samia apongezwe kwa hili.
Kwa wale msiofahamu, moja ya jambo ambalo Mzee huyu alilikiri hadharani tena Waziwazi ni makosa ya kupoka Mali za Sekta binafsi kama vile Mashamba ya mkonge, Pamba, Kahawa na kuyarudisha Serikalini, hili lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi mtakumbuka kabla ya hiki Tanzania tulikuwa ndio vinara wa uzalishaji Mkonge duniani leo majibu sote tunayo.
Swala jingine ambalo Mzee alijutia baada ya kung'atuka madarakani ni kuufanya ushirika uendeshwe na Serikali badala ya kujiendesha wenyewe kama Sekta binafsi nadhani madhara haya hata leo bado yanaonekana japo tunayo nafasi ya kurekebisha.
Wakati flani nikimkumbuka Hayati Mwl JK Nyerere, nikikumbuka maono yake hasa haya ya Ubia huwa napata faraja sana ninapomwona Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipita mulemule na hii ni baada ya miaka 60 kupita.
Hoja fikirishi zaidi kwa wasomaji wangu ni hii, "Kama Muasisi wa Taifa hili hakuwa na Wasiwasi juu ya hii PPP wewe unayesema PPP ni mbaya unalegacy gani kwenye hili Taifa?
===