Kumbe bodaboda wanashirikiana kuiba na kukwapua barabarani

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
11,422
Reaction score
6,108
Kijana mmoja ameporwa simu barabrani tena kwenye service road wakati anaongea,
bodaboda kaipitia kama kipanga,

wakati jamaa anapiga kelele huku anafukuzia akakutana na kijiwe cha bodaboda mbele yake akawaambia naomba mmoja tumfatilie yule mwizi nitalipa hela yeyote, kwa mshangao wote pale kituoni wakakataa

Ikapita bodaboda nyingine akisimamisha na kumuambia tumfukuzie yule jamaa pale mbele amenipora simu nae akakataa, sasa ni wazi kumbe ni ushirikiano maalumu bila shaka
 
Hata mimi ningekataa, risk ya kumfukuza mtu na kupata ajali ni kubwa kuliko pesa utayomlipa huyo boda. Hiyo ni kazi ya police na unamfukuzaje mwizi barabarani bila king'ora.
 
Nazungumzia dar es salaam mjomba , sizungumzii liwale wala mtwara wala popote pasipi na msongamano, ni pembezoni mwa city mall, na foleni iliyopo pale unaijua?
Any way inawezekana na wewe ni bodaboda
 
Kijana mmoja ameporwa simu barabrani tena kwenye service road wakati anaongea,
bodaboda kaipitia kama kipanga,

wakati jamaa anapiga kelele huku anafukuzia akakutana na kijiwe cha bodaboda mbele yake akawaambia naomba mmoja tumfatilie yule mwizi nitalipa hela yeyote, kwa mshangao wote pale kituoni wakakataa

Ikapita bodaboda nyingine akisimamisha na kumuambia tumfukuzie yule jamaa pale mbele amenipora simu nae akakataa, sasa ni wazi kumbe ni ushirikiano maalumu bila shaka
Wizi wa namna hii wenyewe wanauita kwa jina la 'Vishandu.'
 
Kwanza wewe ni jambazi unashirikiana na huyo boda unayemwita mwizi, unataka nimfukuzie mwisho wa siku mnibananishe kona muibe na pikipiki yangu, anyway kwanini akuibie karibu na kituo cha bodaboda?
 
Back
Top Bottom