mwanike wa ukaya
Senior Member
- Feb 3, 2017
- 115
- 79
Habarini wanajukwaa. Kwanza nitoe pongezi sana kuwepo hii forum kwani imenisaidia mengi sana hadi mda mwingine nikikaaga kuwaza kwanini nilichelewa kuwepo humu ila tatizo sio Mimi ni mazingira na uchumi
Stori iko hivi!___
Sikuwahi waza kuna dar kuzurula bila kazi ,au nikae siku moja na kurudi hapana ila nlitamani nikae muda mrefu ili nilijue jiji na sikua na jinsi nyingine zaidi ya Kusoma na namshukuru Mungu mama ndalichako ameona kuwa ninazo sifa za kusoma huku
Nilipofika nlikuwa naogopa na kuiona dar kama ulaya lakini nikajikuta siku nimeanza kupazoea
Kuna siku nliona ni vyema nielekee taifa kuwacheki yanga ya darisalama na ndipo wahuni wakaimezea smartphone yangu iliyokuwa inaonekana Kwa mfuko Wa suruali na nashkuru Mungu katika harakati za kuichomoa nikashtuka na kutumia kaujanja nlikokapata jeshin nkaichukua nikawa nimesalimika
Shida Jana kuna jamaa kaniambia nimsindikize kariakoo kununua Samsung Galax si unajua yeye katokea town kidogo kuliko Mimi interior ....Tukafika Salama tukataka kununua dukani ila kabla hatujaingia akaja teja .mmoja alikua na Galax mashine ...kaifunga Kwa Rambo kajifanya kakwapua na anataka laki duh.. Tukaona ni neema kwetu kwani bei yake ilikua simple .. Tukashauriana kidogo ikabidi jamaa achome walet na kumpa ..tukapotea ..baada ya dakika chache jamaa kaniambia mbona ile soap. Dah. Sikuamini. Dah ama kweli mjini kuna wajanja ...
Tunaomba semina ya nguvu Kwa govt jamani hali sio nzuri ... Watanifanya niwe nashinda ndani kwakweli. Dah.... Mimi mshamba toka k..........