Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

Makavu Ya Leo: Masikini Akipata ------ Hulia Mbwata, bwana mdogo Diamond mtoto wa Tandale ambae wakati Wema Sepetu anakuwa miss yeye alikuwa anauza mitumba kule Tandale kapata pesa sasa naona makalio yake yanalia Mbwata.

Kama unampenda sana Diamond usipanic endelea kusoma utanielewa tu Diamond amewakera mashabiki ndio maana yamemkuta yale yaliomkuta pale Leaders.

Kijana Diamond alikuwa moja kati ya watu masikini sana nchini, alikuwa ANALALA kwenye mazingira magumu ila leo amediriki kusema kuwa MBEYA HAKUNA HOTELI YENYE HADHI YAKE, hahahaa inachekesha sana. Anasahau kuwa umaarufu wake umekuja kwasababu mashabiki WALIAMUA kumkubali.

Wema Sepetu wakati ana make headlines akiwa Miss Tanzania hakuwa anatambua kuwa pale mitaa ya Tandale kuna kijana anaitwa Nassibu anauza mitumba, na ninaamini hata kama angeonana na Diaomnd kipindi kile HAKIKA asingemuangalia mara mbili.

Ila dogo leo kapata hela anaanza kuleta dharau kwa mashabiki. Dogo ana kauli chafu sana, anapenda kujikweza.

Ukitaka ufanikiwe na ufaidi kuwa msanii bongo hakikisha UNAWAFURAHISHA mashabiki wako mdogo wangu.

Waache watu wakusifie wewe. Kitu ambacho hujui ni kwamba hapa bongo kulikwa na wasanii wakubwa kama akina Mr. Nice lakini walilewa sifa na sasa wanaishia kucheza pool pale Sinza Ambiance na kutia huruma.

Usipoangalia wewe na kaka yako Nice mtakaa kijiwe kimoja na kusema ZAMANI NILIKUWA MAARUFU.

Diamond umekuwa na tabia ya kusema wewe ni maarufu na kukataa mara kadhaa (HATA UKIOMBWA) kufanya show sehemu mbali mbali, unajiona ni msanii wa kufanya SHOO ZA MILL 30, kuna cases kadhaa za wewe kuwatolea nje mashabiki kufanya shoo eti kwa madai unataka hela nyingi.

Unasahau watanzania hawa hawa ndio waliokupigia kura ukapata hizo tuzo na kuwa nominated hata kwenye hizo BET, lakini naona sasa UMEUCHOKA umaarufu wako na uko tayari kuupoteza kwa upuuzi tu usio wa maana.

Kuna mambo mengi sana unakosea kama binadamu ila kuna mengi unayafanya makusudi kwasababu wewe ni LIMBUKENI, kwa mfano suala la kutoka na mabinti kadhaa wa kadhaa kwako umeona kama ni ufahari hivi, kumbe wenzako wanakuona zuzu tu maana huwezi kuwamaliza mabinti wote duniani.

Na kwasababu hiyo ndio maana wanaume wenye akili WAMEMUHONGA WEMA GARI wakasingizia kuwa ni Kadinda ndie alietoa, ukiacha dharau watu watakuheshimu.

Sijui niendelee au niishie hapa?! Aah nikiishia hapa ntakuwa nimekuogopa. Mdogo wangu wewe kimziki sio kwamba uko juu sana kuliko Alikiba, Linex, Barnaba, Ben Paul au hata Lady Jaydee ni kwamba umepata promo nyingi sana kiasi cha mashabiki KUAMUA kukukubali.

Unashangaa watu pale leaders waliamua kukuzomea ni kwasababu watanzania wamechoka na majivuno yako na dharau.

Sasa T.I anataka kufanya collabo na Ali Kiba ile inaonesha dhahiri kuwa wewe BADO.

Anyways kama umemaindi poa ila hayo ni maoni yangu kama SHABIKI na ungekuwa wewe ni chama cha siasa hakika leo ningerudisha kadi yangu ya Uanachama mpaka pale utakapojirekebisha!

Usije ukakonda bure kwa makavu haya. La mwisho Gwanda zile zitakuletea matatizo, inawezekana ulionywa hukusikia jaribu tena uone cha mtema kuni.

Next time hutaitwa Oysterbay watakuficha wenye nazo!

Duuh kwel pepo la mr nice la mnyemelea kaka domo
 
1.Mi nna billion moja bank.
2.mbeya hakuna hotel ya hadhi yangu.
3.sifanyi shoo chini ya mill kumi.
4.mimi ni sukari ya warembo.teh
5.nina nyumba nne za bei kali niko namalizia swiming pool.sjui imeshaisha????
6.niko tayari kumsaidia kiba internationally.

Duh,kweli bongo kuna wasanii.
 
Umeshupaa na kutoa povu jingi mdomoni lakini ulichokiandikia ni upuuuzi na upuumbavu mtupu kwani hakuna kitu hapo. Wahenga walisema "mtu mpu.mbavu akikaa kimya huwezi kuujua upumba.vu wake mpaka akiongea" pekee nilichokisoma hapo ni kuwa maelezo yako yamejaa chuki, wivu wa kike , tamaa na roho mbaya.

Swala la Diamond kutokea katika maisha ya kimasikini au dhiki kama unavyosema wewe ingawa huna data zozote za kuthibitisha hilo si jambo la ajabu sana duniani. Tumeona historia za wasanii na wanamichezo na hata wafanyabiashara wakubwa mbalimbali zikielezea jinsi maisha yao yalivyokuwa kabla ya kupata mafanikio kimaisha na ukiangalia wanavyoishi sasa ni tofauti. Haimaanishi kama umetoka katika umasikini basi uendelee kuishi kimasikini labda kwa mtu mwenye umasikini wa kimawazo kama ulivyo wewe. Kwa level ya kimafanikio aliyofikia Diamond si ubishi kwamba yupo katika level za kimataifa na lazima alinde hadhi yake aliyokuwa nayo ili aendelee kuongeza heshima yake na kubwa zaidi kuongeza thamani ya kazi zake na kujipatia fedha nyingi zaidi.

Kubali au kataa Diamond siyo wa kumualika katika vitamasha vya vichochoroni vya kiingilio chupa ya pombe na yeye aende huko ni kujishusha hadhi na kuharibu soko la kazi zake. Alafu hicho kinachotokea sio yeye bali ni nguvu ya soko kwani principle za demand and supply zinasema wazi " the higher the demand the higher the price" sasa demand ya Diamond ipo juu sana hivyo lazima na bei yake nayo iwe juu sana vile vile.

Ali Kiba anajitahidi kuimba lakini ni upumbavu kudhani kwamba unaweza kuiongeza thamani ya Ali Kiba kwa kulazimisha kuishusha thamani ya Diamond.

Sisi washabiki wa Diamond wala hatukasiriki jinsi kijana anavyoringia talent yake kwani ile resource ya thamani kubwa aliyokuwa nayo na lazima aringie ni sawa na Daktari Bingwa anapotaka mshahara mkubwa kwa kuringia elimu yake au Prof. Anapotaka chuo kimlipe fedha nyingi na yupo tayari kufundisha vyuo vyenye hadhi na majina makubwa anaringia taaluma yake. Kwanini unataka Diamond ajitoe bure tu.

Kuhusu mapenzi yake na Wema hayo ni maswala binafsi sana na yanahusu mapenzi siyo kazi. Sasa wewe ulitaka aje kukuoa wewe?

Mwisho nakushauri kama unataka utajiri fanya kazi kwa bidii kwani chuki au tamaa au wivu wa kike hautokusaidia kitu.

Taratiiiiiibu punguza munkar.pamoja sasa eeh?haaya.


Nani anamshusha diamondi ili kumpandisha kiba??,kivipi??.naomba ufafanuzi mkuu.
 
Diamond ni typical Muha na Waha ndivyo walivyo. Wale ni sawa na mbilikimo au watu wafupi, wanapenda sana mabishano hata kama hawako sahihi na nyodo kwao ni haki yao. Kule Kigoma Muha akibahatika kuuza viazi vitamu, mafuta ya mawese, dagaa lazima atawatambia wenzake huku akijuwa kuna pia kuuza genge kesho. Nili enjoy vituko vyao wakati naishi Ujiji na Kasulu for two years.
 
mengi umeongea ni ok lakini sikubaliani na wewe issue ya kupiga show kwa pesa ambayo hamjakubaliana, uamuz wa kupiga show kwa ela gani its purely business si issue ya kufurahisha watu tu...... kama ktk mazungumzo hamjafikia dau flan its ok nothing personal hakuna haja ya kupeana presha za kusingizia mashabiki au kusema ana dharau!!!
 
Jamaaa Mbishi:...xaxa wewe unawaxema wakule wote...cz wakigoma niwengi wako kwenye fan hiyo
 
Mm nahisi mtoa mada ni mvivu wa kufikiri na nina wasi wasi na maarifa yake aliyoyapata darasani.
 
Nawapa mwaka mmoja mtakuja kuniambia kama mtamsikia huyo Diamond maana hatosikika kabisaaa Alikiba now kila mtu anamsaidia maana wameshaona kwa Tanzania mtu wa kupigana na Diamond ni Alikiba na hii yote wanafanya kumuonyesha dunia huwa inabadilika na dharau hazifai.....subirini muone tu....

Wangemsaidia kupanda chati kipindi hicho alipofanya kolabo na R Kelly. Fulsa alikuwanazo lkn akili yake ilikuwa imedorora. Sio kama mwenzake akapata fulsa katumia effectively na kachukua hadi tuzo. Vp Alikiba kashachukua tuzo za kimataifa kama mwenzake?
 
Hata mimi hakuna hotel ya hadhi yangu. Ni swala la standard tu, kila mtu ameset standard yake ya maisha. Kama hakuna 5 star hotel utamlazimisha alale kwenye lodge zenye mbu? ....
 
Makavu mpeni lakini mtoto anajituma. Usipojisifia binadamu wabishi kukusifia
 
Back
Top Bottom