Kumbe DP World wako mabara yote; Tanzania kuna nini?

Kumbe DP World wako mabara yote; Tanzania kuna nini?

Mwanzoni zilipotoka habari za kuwepo mkataba wa bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP world nilifikiri hii ni kampuni ya kijanja janja inayoanza shughuli zake nchini.Baadae ilipokuja hoja ya kuwa ni kampuni ya waarabu nikajua athari ya elimu zitolewazo Tanzania.
Nilipojaribu kuangalia historia na utendaji kazi wa kampuni hiyo nikaono kumbe ni kampuni kubwa sana,iliyoanza kazi miaka kadhaa nyuma na kwamba inaendesha shughuli za bandari katika mabara yote na katika nchi zilizoendelea kama Marekani na ndio wapakiaji wakubwa wa ngano za Ukraine pia zikaifikia dunia nzima kiurahisi.
Ramani na kupanuka kwa shughuli za DP world kila siku zinaongezeka mpaka kufikia nchi hata zisizokuwa na bahari.
Zaidi ni kuwa makao makuu yake yako kwenye nchi ya kiarabu lakini viongozi wake na teknolojia wanazotumia havina sura ya uarabu jambo ambalo ni hoja kubwa ya wapinzani wake.
Kama kuna watu wanaopinga mkataba huu kwa maoni yangu wabadili hoja zao zielekee kwenye marekebisho penye mapungu na si kupinga au kutumia kipengele cha uarabu.Wakifanya hivyo watadharaulika na hawataaminika katika misimamo yao mingine ya kisiasa.Kwa upande mwengine wakisikilizwa na kuachwa mkataba huu basi watazifanya bandari za Tanzania ziwe kama zilivyokuwa karne iliyopita.Zitakuwa kama bandari za kusubiria samaki na majahazi,Meli za mizigo zitaelekea nchi nyengine.
Pitia mkataba wetu na dpw, ufananishe na mkataba wa UK na dpw.
Hakuna anayempinga muarabu katika bandari au mzungu katika madini, ila mikataba ya kinyonyaji na kandamizi kwa utawala na ustawi wa nchi.
 
Unajitoa ufahamu? Kwani tunajadili mkataba gani? Haya, tunajadili mkataba wa bandari kati ya Tanganyika na DP World. Nataka kuulinganisha huo mkataba walioingia Tanganyika na DP World na mikataba abayo DP World imeingia na nchi nyingine Dunianai kama hiyo mikataba ina matongotongo kama wa Tanganyika.
Huo mkataba wa uendeshaji bandari uko wapi?
 
Tatizo si ufanyaji kazi wa hiyo kampuni, tatizo ni makubaliano yaliyomo kwenye huo mkataba.
Siamini kama mikataba yote iliyongiwa kati ya hiyo kampni na hizo nchi inafanana mkataba wa hapa TZ
Sahihi..
MIKATABA..
MKATABA..
 
Back
Top Bottom