Pamoja na kwamba kina Jefferson walisema hivyo huku wengine kwa wakati huo huo wakimiliki watumwa, ukweli wa dhana hiyo unabaki pale pale. Walichobugi wao ni kutotenda walichohubiri au kuandika.
Haya ni maneno mazito sana; Wakati Marekani inaundwa kama Taifa mwaka 1776 hawakutoka kwenda kujenga Taifa la watu walio sawa. Sisi (chini ya Mwalimu) tulikuwa na maono ya kwenda kujenga "Taifa la watu walio huru na sawa".
Tofauti kati ya Azimio hilo la Marekani na letu la Arusha ni kuwa sisi ya kwetu ilikuwa ni dira. Tulitaka tuwe na Taifa la namna gani na tukatoka kwenda kulijenga. We were and still remain the only country in Africa which had an articulated vision of what kind of nation ilitaka iwe na ikatoka kwenda kujaribu kulijenga.
Ndio maana mwanzoni baada ya uhuru sisi tulikuwa na kitu ambacho kinaitwa "kujenga Taifa" (Nation Building). Watu wengi wanachukuliaa kwa maana ya kulitumikia Taifa (National Service). The later came from the former.
Tulipopata uhuru hatukuwa na nchi au taifa. Tulikuwa na eneo ambalo liiko chini ya uangalizi (a territory). Hili linawezekana watu wasilielewe vizuri. Wajerumani walipochukua eneo la Afrika ya Mashariki katika uvamizi na kugawana kwa Afrika kwa 1885 kule Berling wao hawakujali ni nini wakaamua kugawana eneo la Afrika ya Mashariki kati yao Wafaransa, Wabelgini, na Wareno na Waingereza.
Kilichosimamia mgawanyo huo ni vitu viwili hasa kile cha "sphere of influence" na mwenye kuwahi kupata basi anachukua. Na hata baada ya Ujerumani kupoteza koloni (siyo nchi au taifa) Waingereza walipwa na Umoja wa Mataifa (then League of Nations) eneo hilo lililokuwa la Mjerumani likawa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa. Na hilo ndilo likadhaniwa kuwa litakuwa sehemu ya nchi mpya ya Tanganyika.
Ilikuwa ni hekima ya Nyerere na viongozi wengine wa OAU kuamua kuheshimu mipaka ya kikoloni kama msingi wa mataifa yao mapya licha ya ukweli kuwa mipaka hiyo haikuzingatia hali halisi ardhini. Matokeo yake ni jinsi makabila na jamii mbalimbali zilivyojikuta zikimegwa na kuwa sehemu ya taifa zaidi ya moja.
Hivyo inapokuja Disemba 9, 1961 Nyerere alichopokea hakikuwa nchi wala Taifa. Siyo kama Mandela alivyochukua Urais wa Afrika ya Kusini kwani tayari ilikuwa ni nchi. Alichopokea Mwalimu usiku ule wa kukumbukwa na mkusanyiko wa makabila na jamii mbalimbali za watu ambao waliunganishwa siyo na dhana, lengo, au mwelekeo mmoja; hapana bali waliounganishwa na maslahi ya wageni (wajerumani na Waingereza baada yao).
Na hapa ndio unaweza kuona ni kwa jinsi gani TANU chini ya Nyerere ilitumia muda mrefu sana kuunganisha nchi chini ya sera na itikani yenye kuvutia watu wengi zaidi na mwelekeo mmoja.
Sasa hapa tunajiuliza; Nyerere anapokuwa Waziri Mkuu na baadaye Rais:
a. Jukumu lake la kwanza lilipaswa kuwa nini?
b. Akiwa katika kupanga kutekeleza jukumu hilo anakutana na njaa ya 1962, yeye kama kiongozi jukumu lake la kwanza ni nini?
c. Wakati hako kataifa hakajafika mbali rafiki na mpambanaji mwingine Patrice Lumumba anauawa mashariki mwa Tanganyika na Congo inakuwa matatani, Nyerere jukumu lake la kwanza ni nini?
d. Kabla hajatulia yanatokea mapinduzi ya Zanzibar, haka ka nchi ka Tanganyika chini ya mwalimu jukumu lake la kwanza ni nini?
e. Kabla hawajakaa sawasawa Jeshi linaasi na kusababisha umwagikaji damu, jukumu la Rais wakati huo ni nini?
f. Wakati hayo yote yanaendelea vita baridi inakuwa imepamba moto duniani, bado nchi kadhaa zinazotuzunguka ziko katika ukoloni Msumbiji, Namibia, Zimbabwe n.k jukumu la Nyerere ni nini?