wandugu kwenye siasa au ungwini hakuna aliye sahihi na ambaye si sahihi, kilichopo ni kujenga hoja na kuitetea hoja.
Kikwete amewahi kutofautiana kikauli na lowassa mara nyingi, mojawapo ikiwa ni ile ya "mamilioni ya jakaya". Lowassa alitaka watendaji wa benki wasilete urasimu wa kutoa fedha zile, na kikwete akasema fedha zile ni mikopo, na taratibu zote za kibenki za kugawa mikopo nafuu zifuatwe, na hakuna kugawa fedha kiholela holela. Ni hoja tu, na jinsi mtu anapoweza kuzijenga na kukubalika.
Na wakati mwingine mwenye kisu kikali ndiye mla nyama, na jk ana kisu cha urais, na mara nyingi yeye husema mwishoni.