Kumbe Jk Bado Mtu wa Watu!

Kumbe Jk Bado Mtu wa Watu!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,147
Kutokana na ambayo nimekua nikiyasoma humu kuna wakati nilianza kuhisi labda JK Si kipenzi cha watanzania wengi tena,hii ni kutokana na watu walio wengi humu kumuongelea vibaya,leo nimejiridhisha kwamba kumbe na kakikundi ka watu wachache tu ndiko kanakopotosha watu humu kwa sababu maalum,lakini huko "site" jk anaonekana kuwa mwanasiasa pendwa pengine kuliko yeyote yule na wapiga kura.........!

Kumbe jk bado mtu wa watu hili utaweza tu kuliona kama wewe ni katika wale wanaoamini wanachokiona na si kuona kile tu wanachokiamini wao!

Nawasilisha kimtindo!






 
Mkuu hapo ni msibani,na kwenye msimba lazima kila mtu aweke tofauti yake pembeni.
 
msanii na wasanii!
Namuona dr cheni,ray na wasanii wengine kibao wakimpokea kwa bashasha!
 
Cheap popularity, mambo nyeti ya mstakabali wa taifa haonekani lakini mambo ya kipuuzi kama kuhani msiba ya mwana maigizo mbakaji wa under 18 anakwenda
 
Mkuu hapo ni msibani,na kwenye msimba lazima kila mtu aweke tofauti yake pembeni.

wanaweka tofauti pembeni na kugombea kushikana nae mkono sio!ok it sounds good kama ni hivyo,tumekomaa kidemokrasia
 
Jk sio mdini kama viongozi wachadema slaa na wengineo lazima awe nimtu wa watu
 
Cheap popularity, mambo nyeti ya mstakabali wa taifa haonekani lakini mambo ya kipuuzi kama kuhani msiba ya mwana maigizo mbakaji wa under 18 anakwenda
Issue ni jinsi mkono wake unavyopiganiwa na wapiga kura,acha upotoshaji wa makusudi kuharibu lengo
 
Cheap popularity, mambo nyeti ya mstakabali wa taifa haonekani lakini mambo ya kipuuzi kama kuhani msiba ya mwana maigizo mbakaji wa under 18 anakwenda

hana adabu kabisa huyu jamaa,anadhan atatatua umeme kwa kwenda msibani
 
Kwa position yake kama rais wa jamhuri wa Tanzania yeye ni selebrite ambaye anapatikana kwa nadra sana. Kwa hiyo hataka kama hukubaliani na sera zake, unaweza kutaka kukutana kupiga picha na hata kushikana mikono na selebrite huyo. Huenda hata mimi ningekuwapo msibani hapo ningependa kutumia nafasi hiyo kushikana naye mikono na hata kupiga picha naye ingawa najua kuwa ni rais bomu.


Kwa upande mwingine sidhani kama kitendo chake cha kwenda pale kilikuwa cha busara sana kutokana na position yake. Kuna watanzania raia wengi wanaokufa kila siku na huwa hahudhurii misba yao, kwa hiyo kuhudhuria misiba ya raia selectively kutokana na umaarufu wao nadhani ni upungufu wa maono. It is possible alikuwa anahitaji sifa kutokana na coverage ya msiba huo, lakini ni sifa ambayo siyo nzuri
 
Ala kumbe...!, asante kwa taarifa, (as if aliwahi kuwa sio!)!.

kweli wachaga mtachukua muda mrefu sana kukijua kiswahili,mkuu limetukia neno "BADO" (ni mtu wa watu)sijui kama unajua matumizi ya neno hilo,ningejua lugha yenu pengine ningekuandikia kwa kichagga may be ungeelewa haraka
 
Kwa position yake kama rais wa jamhuri wa Tanzania yeye ni selebrite ambaye anapatikana kwa nadra sana. Kwa hiyo hataka kama hukubaliani na sera zake, unaweza kutaka kukutana kupiga picha na hata kushikana mikono na selebrite huyo. Huenda hata mimi ningekuwapo msibani hapo ningependa kutumia nafasi hiyo kushikana naye mikono na hata kupiga picha naye ingawa najua kuwa ni rais bomu

Alaa! ok
 
hana adabu kabisa huyu jamaa,anadhan atatatua umeme kwa kwenda msibani

kwa hiyo ulitaka ahamishie ofisi ya rais na ikulu nzima TANESCO na awe anashinda kwenye mitambo ya umeme au
 
Hao ndiyo wenzie kwa kuwa wote ni wasanii tofauti ni kwamba usaniibwa JK unafanyikia Magogoni wakati akina Dr Cheni wanafanyia Leaders club.
 
Back
Top Bottom