Kumbe kitunguu saumu kinalipa hivi

Kaka interest yangu ni tangawizi. Nipo Makambako ipo siku nitakuja hapo Igawa. Napenda kilimo sana. Mashamba yangu yapo Mambi Igurusi
 
Pl hujaongelea gharama zake mku
Plus estimation za mavuno kwa ekari na bei yake
 
Hz gharama zake zikoje?
tuseme bei ya 300,000 hadi 500,000 kwa gunia na kupanda gunia 16 hadi 28 kwa ekari unaapata gharama za mbegu 4.8m hadi 14m. madawa, vibarua na mbolea sina uzoefu washambani. ngoja tuwasubiri watu wa babati.
 
Mkuu kisima nilikua nakuheshim sana but hii comment yako sio ya kiungwana kabisa
Hv ni lazima ulete data humu?we toa msaada the rest ni mtu mwenyewe anajua
Kwanza unajuaje kama mtu hajalima?kwani ni dhambi kuulizia data zingine zaidi ya kilimo unachofanya?huwez kua na plan za baadae?ts a shame mkuu umefanya ujinga wa kiwango cha lami mkuu jifunze kuheshime mawazo hayo hayo unayoona ya kijinga sababu hatuna plan sawa
Hatuwez wote tukashinda kwenye majukwaa ya mapenz au siasa so kwa kila mada inayopostowa humu lazima tuulize maswali na kupata uelewa wa kutosha kama unaona hupend tunavyopata elimu basi acha kuto msaada hulazimishwi
 
Huku igawa wanakodisha mashamba?na kama wanakodisha kwa gharama gani?
 
Reactions: 365
Kwa Morogoro sehemu gani maeneo ya Kilosa inastawi hii kitu.
 
Nilishawahi kulima vitunguu hapo Igawa nikala mweleka,nikawa bado kwenye maruweruwe nikanyanyuka hku napepesuka nikalima tena nyanya nikapiga mzinga wa haja hata kumi haikurudi
What happened mkuu
 
What happened mkuu
Mbegu za vitunguu zilikuwa fake sana. Kwa nyanya msimu niliilima bwanae zilimwagika mtaani kama mchanga sijui zilitokea wapi unatafuta wateja wala hupati hata mmoja...watu walitelekeza nyanya mashambani sana pamoja na mimi after two week zikaadimika ndo ikawa imekula kwetu tuliotelekeza.

Nikabadilisha,nikalima mahindi nikavuna msimu wa mwaka juzi kama sikosei daaah,ikawa balaa tena mahindi yalikuwa mengi sana msimu ule bei iliporomoka vibaya mno,yaani kwenye kilimo bado sijawa na bahati nayo sana ila kuna moja hiyo ndo nilipiga mzinga mtakatifu vibaya with no any return.
 
Hammer nadhani hapo ulipata hasara ya pesa ila ulipata faida kubwa ya uzoefu, mimi binafsi nimepata hasara mara mbili kubwa za kipesa ila nikapa faida kubwa za uzoefu, kwa mfano ukilima nyanya usilime shamba zima kwa mpigo kama ni heka tano basi kila heka ipishane na nyingine kwa muda mwezi mzima wakati wa kupanda, ili utapoanza kuvuna heka moja ikikutana na bei mbaya sokoni basi heka inayofuata lazima ikutane na bei nzuri sokoni sababu bei mbaya ya nyanya hua haidumu za zaidi ya wiki tatu.
 
Mkuu naomba usinichoke kwa maswali yangu
Wanna knw ulikosea wp tofauti na unachokisema
Nyanya ulilima miez gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…