Mkuu naomba usinichoke kwa maswali yangu
Wanna knw ulikosea wp tofauti na unachokisema
Nyanya ulilima miez gani?
Kwanza uchaguzi wa mbegu bora ni muhimu sana,kwenye vitunguu niliuziwa mbegu fake.
Then kwa kilimo cha mazao yanayooza, kabla ya kulima jaribu kufanya survey ya maeneo yanayo-supply mazao hayo kama wamelima kwa kiasi gani. Mimi nilipata hasara kutokana na msimu niliolima nyanya watu wengi sana walilima zao hilo kiasi kwamba mtu anataka debe moja kwa 1500 tena kwa mkopo.
So,sio kama ina msimu maalum ya kulima nyanya ila wewe ukishakabidhiwa shamba ndo utaamua unalima vitunguu,nyanya,hoho,mahindi au viazi.
Mfano kulima vitunguu kuanzia mwezi January ni gharama na wengi hawalimi miezi hiyo kiasi kwamba April na mwezi May mwanzoni bei kwa gunia la kilo 100 inafika 150,000/= hadi 200,000/= but ikifika mwezi March wengi wanapanda na kivuna mwezi June na kupelekea bei kuwa Tsh.30,000/= hadi 50,000/=.
Kwa hiyo unaona kabisa bei inashushwa na wingi wa bidhaa. Hivyo ukifanya timing nzuri unapiga faida kubwa sana ila ukibugi ndo madhara unayapata hasa kwa nyanya ambayo huwa inaharibika kwa kuoza isipochumwa mapema.
Hope umenipata kidogo!