Thanks kwa taarifa, mbona hata vyombo vya habari havijatamka juu ya hilo. Tupatie majina yao tuwajue "MATRAITORS".
JAMANI ujinga huu haujaanzia hapo tu, lazima tufuatilie tujue tabia zao toka utotoni na hata walipokuwa shuleni walikuwa ni watu wa aina gani.
hili ni funzo tunapochagua viongozi tusisome CV zao tu, maana CV za utotoni huwa hawaziweki.
Wengine unakuta walikuwa ni kina "TOTO TUNDU" waioambilika.
Wengine "TOTO JOGA" likigomwa kidogo tu Kiliooooo hadi majirani wasikie
Wengine " TOTO DEKA" kila kitu ng'eee ng'eee mama mie nataka ileee, mmm hii sitaki mama nataka ileeee!
wengine "TOTO JIZI" mama na baba wakiondoka nyumbani kazi kupekua masanduku au kuramba sukari.
sasa tusikurupuke kuchagua viongozi kwa kuangalia CV zao za masomo tu haya ndio matokeo yake.
kumbuka hata mashuleni tulipokuwa tukisoma, ukiwekwa msimamo fulani unakuwa wengine wanasepa haoooo huwaoni, au wale wanafunzi wa kujipendekeza, yaani likimwona teacher na mkoba, utaona hilo mbio kwenda mkumpokea, "shikamoo mwalimu".
VIJITABIA ni Kadhia kubwa inayotukabili ktk viongozi wetu wengi maana hawajaviacha vijitabia hivyo hadi sasa.