John Einar Selander alikuwa mkurugenzi wa idara iliyokuwa inajulikanakaa PWD, yaani Public Works Department, wakati wa utawala wa kikoloni. Alisimamia ujenzi wa lile daraja kuelekea Oysterbay ambayo wakati huo ilikuwa inaitwa uzunguni. daraja lile lilikuwa dogo ambalo wakati wa mvua lilikuwa linapitika kwa shida shida. Kwenye miaka ya sabini wakati Nyerere akiwa Japan, alipewa zawadi ya ujenzi na mfalme wa Japan, yeye akaomba ajengewe "daraja" kama yaliyoko japan. Wakati ule mfalme alidhani kuwa Nyerere anaomba ujenzi wa Daraja kuunganisha Dar na Zanzibar akama ambavyo wajapani wameunganisha visiwa vyao kwa madaraja, hivyo akaiagiza serikali ya Japan ilete mkandarasi wa hali ya juu kufanya kazi hiyo kulinda jina na heshima ya mfalme. Serikali ya Japan ikaleta kampuni ya Kajima ambayo ilikuwa kampuni kubwa sana ya ujenzi kuliko zote wakati huo na ilikuwa imeshiriki ujenzi wa madaraja mengi ya kuunganisha visiwa vya Japan. Wahandishi wa Kajima walipofika wakaambiwa ni ujenzi wa Selander Bridge vizuri kati ya Msasani alikokuwa akiishi Nyerere na Ikulu, ni jambo ambalo lilikuwa kama kichekesho kwao. Ila waliona kuwa miundo mbinu Tanzania ilikuwa ni mibovu sana, wakati Japan ikiwa inapanua masoko ya uuzaji wa Magari kwa hiyo wakadhani kuna uwezekano wa kupata kandarasi nyingi za ujenzi huko mbeleni. Wakaweka ofisi yao Tanzania na waliendelea kuwapo kwa muda mrefu kidogo ingawa baadaye miradi ikawa inafanywa na Konoike.