Kumbe lile daraja pale Kindondoni linaitwa Selander Bridge?

Kumbe lile daraja pale Kindondoni linaitwa Selander Bridge?

Limeandikwa kwenye kibao cha shaba SELANDER BRIDGE,uwe unadoma soma,mambo ya kusikia sikia ndiyo yaliyozaa maneno kama"KOLOBOI"badala ya "Call boy"ikimlenga jamaa wa zamu anaekaa na taa usiku kwenye makutano ya barabara na reli,ambapo hata kwa mchana anakuwa na kibendera ambapo hakuna taa rasmi za kuashiria.
 
Story nzuri na inafurahisha ila matukio hayapo clear.

Je, huyo Selander ambaye kwa jina imaonyesha alikuwa na asili ya Uingereza alikuwa mfanyakazi enzi za mkoloni, ina maana alikuwa anafanya kazi kwenye utawala wa Nyerere miaka ya '70? Kama ni hivyo, kulikuwa na haja gani kusema 'alikuwa ni Mkurugenzi enzi za mkoloni' wakati tunaongelea miaka 10 baada ya uhuru?

Na kwa nini Nyerere aliona busara kulipa daraja jina la huyo Selander wakati ufundi na pesa za ujenzi zilitoka kwa Mfalme wa Japan? Mwenye ufahamu wa hayo aendelee kutiririka.

Na kusema Nyerere alivyokuwa na uwezo wa kujielezea alishindwa kujielezea kwa ufasaha Mfalme hadi ikadhaniwa anaongelea daraja la Zanzibar nalo ni ngumu kuamini. Hizi taarifa alikuja kuzitoa nani?
Daraja lilijengwa kwa mara ya kwanza na wakoloni, likaitwa Slander Bridge.

Nyerere alipohamia Msasani, likawa ni dogo na lina kero nyingi ndipo akaamua kulijenga upya na kulipanua bila kubadili jina. Kuna majina mengi sana yaliyoachwa na wakoloni bado tumeendelea kuyatumia kwa muda mrefu sana; mfano Ocean Road ilibadilishwa majuzi tu kuwa Barack Obama, na Oyster Bay bado mpaka leo tunaiita hivyo hatujaibadili.

Nyerere hakuomba kitu ila alishtukizwa zawadi ya kujengewa kitu, yeye akaamua kujengewa daraja. Detail za ujenzi zilifuatia baadaye. tena afadhali yeye aliomba daraja tunalotumia wengi, miaka ya hivi karibuni kuna watu wangeomba wajengewe ghorofa Tokyo hapo hapo.
 
John Einar Selander alikuwa mkurugenzi wa idara iliyokuwa inajulikanakaa PWD, yaani Public Works Department, wakati wa utawala wa kikoloni. Alisimamia ujenzi wa lile daraja kuelekea Oysterbay ambayo wakati huo ilikuwa inaitwa uzunguni. daraja lile lilikuwa dogo ambalo wakati wa mvua lilikuwa linapitika kwa shida shida. Kwenye miaka ya sabini wakati Nyerere akiwa Japan, alipewa zawadi ya ujenzi na mfalme wa Japan, yeye akaomba ajengewe "daraja" kama yaliyoko japan. Wakati ule mfalme alidhani kuwa Nyerere anaomba ujenzi wa Daraja kuunganisha Dar na Zanzibar akama ambavyo wajapani wameunganisha visiwa vyao kwa madaraja, hivyo akaiagiza serikali ya Japan ilete mkandarasi wa hali ya juu kufanya kazi hiyo kulinda jina na heshima ya mfalme. Serikali ya Japan ikaleta kampuni ya Kajima ambayo ilikuwa kampuni kubwa sana ya ujenzi kuliko zote wakati huo na ilikuwa imeshiriki ujenzi wa madaraja mengi ya kuunganisha visiwa vya Japan. Wahandishi wa Kajima walipofika wakaambiwa ni ujenzi wa Selander Bridge vizuri kati ya Msasani alikokuwa akiishi Nyerere na Ikulu, ni jambo ambalo lilikuwa kama kichekesho kwao. Ila waliona kuwa miundo mbinu Tanzania ilikuwa ni mibovu sana, wakati Japan ikiwa inapanua masoko ya uuzaji wa Magari kwa hiyo wakadhani kuna uwezekano wa kupata kandarasi nyingi za ujenzi huko mbeleni. Wakaweka ofisi yao Tanzania na waliendelea kuwapo kwa muda mrefu kidogo ingawa baadaye miradi ikawa inafanywa na Konoike.
Niongezee hapo, mkabala na Kanisa la St. Peters hapo kuna Shule ya Mbuyuni. Wakati wanajenga pale Selander, Vifusi vya kokoto vilitokea hapo bondeni pembezoni mwa Shule ambayo ilibarikiwa kuwa na Walimu wa watu al-maarufu Tanzania mmoja wapo akiwa Mama Janet M.
Kwaavile ulikuwa uwanja wa shule, baada ya kumaliza kutifutifua hapo, walilazimika kama sio kulazimishwa kuusawazisha na hata kuongezea udongo pamoja na mchanga.
Hapo uwanjani kuna mpaka nondo za zamani za daraja lililofumuliwa
Uwanja ule ukaitwa Uwanja wa Kajima na hapo ikatokea timu moja inaitwa Kajima Sports kama sikosei.

Karibu Dism
 
Kwa miaka mingi, nilikuwa naliita hili daraja la karibu na Kinondoni na Upanga kama SURRENDER BRIDGE na nilidhani pia linaandikwa hivyo maana siku zote nasikia linatamkwa hivyo.

Nimepita juzi nikashangaa mabango mawili tofauti yaliyopo kituo cha polisi pale yameandikwa SELANDER POLICE STATION.

Ningependa kujua Selander ina maana gani? Ni jina la mtu au na mbona sijawahi kusikia mtu akilitamka hivyo?
Wabongo wanaita Ostabei
Oyster bay
Oyster= Chaza
Bay= eneo la bahari lililoingia nchi kavu
 
Wengi wenu mnazungumzia NEW SELANDER BRIGE ambalo limejengwa mwaka 1982 kwa msaada wa Japan. Lakini pale pembeni pana daraja la mwanzo OLD SELANDER BRIGE ambalo lilijengwa mwaka 1929 na wakoloni wa Kiingereza na kupewa jina la huyo afisa JOHN SELANDER aliyefariki mwaka 1927.
Wazo la ujenzi wa daraja jil mwaka 1929 ni baada waingereza kuanza kutawala Tanganyika, hawakutaka kuishi maeneo ya upanga ambayo wajerumani waliishi hivyo wakatafuta eneo la Oysterbay na kuanzisha makazi. changamoto ikawa kuvuka huo mkondo wa bahari kwenda Oysterbay, ndipo wazo la kujenga daraja hilo likaanza.
 
Back
Top Bottom