Kumbe machozi ni sumu!

Kumbe machozi ni sumu!

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
257
Siku moja mtoto wangu wakike mwenye miezi 7 alipoamka kutoka usingizini alianza kulia mara baada ya muda machozi yalimwingia masikioni kwani alikuwa amelalia mgongo na dada wa kazi alichelewa kumtoa kitandani,hivyo alilia kwa muda kidogo na baadae akanyanyuliwa mara baada ya masaa kadhaa maskio yake yakaanza kutuo usaha niliogopa sana,mama yake alimpeleka hospitali kupata tiba,hapo ndipo nilipo gundua na kuambiwa kuwa machozi ni sumu pia
 
Najifunza mengi sana humu, iIdumu JF. JSijawahi ufikria hili.
 
Hospital ndio walimwambia au wewe umehisi itakuwa ni sababu ya machozi??
 
Mi nazani wengi ni wageni na hili tatizo ndio maana baadhi mnabisha,jaribu kuuliza kwa wataalam watakujulisha vizuri mi naandika nilicho thibitisha kabisa
 
ni madaktari wa Tanzania tu ndio wanaweza kukwambia hivyo....huwa sismini hata siku moja..
 
Siku moja mtoto wangu wakike mwenye miezi 7 alipoamka kutoka usingizini alianza kulia mara baada ya muda machozi yalimwingia masikioni kwani alikuwa amelalia mgongo na dada wa kazi alichelewa kumtoa kitandani,hivyo alilia kwa muda kidogo na baadae akanyanyuliwa mara baada ya masaa kadhaa maskio yake yakaanza kutuo usaha niliogopa sana,mama yake alimpeleka hospitali kupata tiba,hapo ndipo nilipo gundua na kuambiwa kuwa machozi ni sumu pia
Ninachojua mimi ni sumu kwa wadudu hasa wale wadogo wanaoruka ambao mara nyingine huweza kukuingia jichoni,wale wadudu mara wanapokutana na machozi hufa mara moja,wengi wao hufia jichoni na ni wachache sana hufa baada ya kutolewa.
 
Siku moja mtoto wangu wakike mwenye miezi 7 alipoamka kutoka usingizini alianza kulia mara baada ya muda machozi yalimwingia masikioni kwani alikuwa amelalia mgongo na dada wa kazi alichelewa kumtoa kitandani,hivyo alilia kwa muda kidogo na baadae akanyanyuliwa mara baada ya masaa kadhaa maskio yake yakaanza kutuo usaha niliogopa sana,mama yake alimpeleka hospitali kupata tiba,hapo ndipo nilipo gundua na kuambiwa kuwa machozi ni sumu pia

attachment.php

Mwanamke akilia Preta amlilia Mkuu MziziMkavu.

Ni kweli Machozi yana sumu.

Zipo aina tatu za machozi

Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yasiathiriwe na vumbi na vitu vingine.

Mirija hiyo ipo chini ya kope za juu na huzalisha maji yenye chumvichumvi ambayo ndiyo machozi-hayo husambazwa katika jicho- kila binadamu anapopepesa.
Wanasayansi wanasema,
zipo aina tatu za machozi ambazo huzalishwa na macho ya binadamu.
Yapo machozi yajulikanayo kama
Basal au Basali. Machozi haya yana kazi kubwa ya kulinda jicho na kulipa unyevu.

Machozi mengine ni ya
Reflex haya yana kazi kubwa ya kutoa tahadhari kwa jicho pale linapoumia. Kwa mfano mtu akikata kitunguu au mdudu akiingia jichoni.

Machozi ya hisia au
Pysch haya hutiririka pale ambapo binadamu hupatwa na uchungu, maumivu, msongo wa mawazo au furaha.

Tafiti zinaonyesha kuwa machozi ya hisia yana kiwango cha manganizi, chembechembe ambazo huathiri tabia au roho ya binadamu.

Machozi hayo ya hisia pia yana vichocheo vya prolactini ambavyo husimamia uzalishwaji wa maziwa.

Machozi yanayozalishwa kwa hisia yana mchanganyiko wa kemikali tofauti na aina nyingine za machozi.
Hivyo basi, binadamu anapolia, hutoa manganizi, potashiam na prolactini. Chembechembe hizo zinatajwa kupunguza mshtuko au huzuni kwa kuweka uwiano wa msongo wa mawazo katika mwili. Ubongo unavyofanya kazi hadi binadamu kulia
Kwa kawaida mfumo wa fahamu
(ubongo) kupitia mishipa maalumu ya fahamu huweza kuwasiliana na kutafsiri taarifa mbalimbali za kimwili na kisha mwili hutoa mwitiko baada ya tafsiri.

Machozi yatokanayo na kuhuzunika
(emotion tears) huwa yanaambatana na uso kubadilika kuwa mwekundu, misuli ya uso kukunjika, kutetemeka, pumzi kukatika na mwisho huenda mwili mzima ukakamaa.

Machozi yatokanayo na hali hii ni tofauti ukilinganisha na machozi ya kawaida ya kulainisha jicho, machozi ya hisia huwa na vichocheo aina ya prolactini na adrenocotrico.
Hali hii hudhibitiwa na mfumo usio wa hiyari autonomic system.

Mfumo huu umepenyeza mishipa ya fahamu inayoshusha mihemko ya kimwili (parasympathetic system) katika tezi inayohifadhi machozi kitaalamu inaitwa lacrimal.
Kemikali maalumu ziitwazo
acetylcholine hupitisha taarifa za mfumo wa fahamu, kwenda katika vipokezi vilivyopo katika tezi ya lacrimal iliyopo katika kona ya jicho.
Hapo tezi hiyo hupata mihemko na kumwaga machozi kutokana na taarifa ilivyotafsiriwa katika ubongo kam vile hasira au mtu kuudhiwa.

Mawasiliano
Wataalamu wengine wanasema kuwa kulia au machozi ya hisia ni nyanja ya mawasiliano. Kabla watoto hawajaweza kuzungumza hulia.

Hii ndiyo njia pekee kwa watoto wachanga kueleza hisia zao za maumivu, kuumwa au woga.
Hata hivyo watu wazima hulia ili kujenga ukaribu na wenzao. Kulia kwa uchungu kunasaidia walio karibu nao kuonyesha ukaribu wao na upendo kwako.

Wengine wanadai kuwa kulia husaidia kuondoa kiwango cha sumu mwilini.
Mwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Modesta Kimonga anasema kibaolojia mtu hulia kwa sababu ya vichocheo ambavyo husimamia uamuzi.

Kwa kawaida ubongo wa mtu hupeleka taarifa kuwa mtu anataka kulia kutokana na vichocheo vya lanchrimal anasema Kimonga
Kimonga anasema tofauti ya kulia kati ya wanawake na wanaume husababishwa na mguso wa moyo.

Wanaume hulia kwa kiwango kidogo kwa sababu wana mguso wa chini tofauti na wanawake.
Mwanasayansi wa
Dutch, Ad Vingerhoets ambaye ametumia miaka 20 kutafiti kwa nini na wakati gani binadamu hulia anasema machozi yanamaanisha kukosa msaada.

Vingerhoets anasema kulia ni maelezo ya hisia kwa watu wazima na ni mawasiliano.
Watu wengine hulia ili wapate ukaribu, wabembelezwe na watengeneze uhusiano, anasema
Vingerhoets

Mwanahistoria wa tamaduni, Thomas Dixon anasema machozi wakati mwingine husababishwa na furaha kuliko hasira au huzuni.
Kwa mfano mwanariadha aliyeshinda medali ya dhahabu, mwanamuziki aliyepata tuzo anaweza kulia kwa furaha, anasema

Aina za kulia

Dk Mkumbo anasema watu wametofautiana kiwango cha kulia.
Wapo ambao hulia hata kama wakicheka, lakini wengine ni vigumu kutoa machozi hata wakumbwe na huzuni kiasi gani anasema
Anasema kulia kunatofautiana kulingana na kiwango cha hisia, mila, tamaduni na maadili.
Zipo mila ambazo mwanamume haruhusiwi kulia kwani kulia kunafananishwa na woga. Wanaume wa makabila haya hurudisha machozi ndani na kubeba huzuni kwa namna nyingine anasema Dk Mkumbo.

Kasoro za vilio
Upo ugonjwa kwa kitaalamu unajulikana kama
Bells palsy Kupooza kwa uso kupinda mdomo ambapo neva za uso husababisha mtu kutokwa machozi pindi anapokula.
Cri du chat, ambapo kichanga anaweza kulia sawa sawa na paka. Tatizo hili huhusishwa na mfumo wa fahamu.

Wapo wanaolia lakini machozi hayatoki, huu ni ugonjwa.
Wengine hushindwa kutofautisha matukio ya kulia au kucheka na wakati mwingine yote kwa pamoja.
Ukiwa na Swali lolote unawea kunitafuta kwa kubonyeza hapa.
machozi.jpg
 
attachment.php

Mwanamke akilia Preta amlilia Mkuu MziziMkavu.

Ni kweli Machozi yana sumu.

Zipo aina tatu za machozi

Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yasiathiriwe na vumbi na vitu vingine.

Mirija hiyo ipo chini ya kope za juu na huzalisha maji yenye chumvichumvi ambayo ndiyo machozi-hayo husambazwa katika jicho- kila binadamu anapopepesa.
Wanasayansi wanasema,
zipo aina tatu za machozi ambazo huzalishwa na macho ya binadamu.
Yapo machozi yajulikanayo kama
‘Basal’ au Basali. Machozi haya yana kazi kubwa ya kulinda jicho na kulipa unyevu.

Machozi mengine ni ya ‘Reflex’ haya yana kazi kubwa ya kutoa tahadhari kwa jicho pale linapoumia. Kwa mfano mtu akikata kitunguu au mdudu akiingia jichoni.

Machozi ya hisia au ‘Pysch’ haya hutiririka pale ambapo binadamu hupatwa na uchungu, maumivu, msongo wa mawazo au furaha.

Tafiti zinaonyesha kuwa machozi ya hisia yana kiwango cha manganizi, chembechembe ambazo huathiri tabia au roho ya binadamu.

Machozi hayo ya hisia pia yana vichocheo vya prolactini ambavyo husimamia uzalishwaji wa maziwa.

Machozi yanayozalishwa kwa hisia yana mchanganyiko wa kemikali tofauti na aina nyingine za machozi.
Hivyo basi, binadamu anapolia, hutoa manganizi, potashiam na prolactini. Chembechembe hizo zinatajwa kupunguza mshtuko au huzuni kwa kuweka uwiano wa msongo wa mawazo katika mwili. Ubongo unavyofanya kazi hadi binadamu kulia
Kwa kawaida mfumo wa fahamu
(ubongo) kupitia mishipa maalumu ya fahamu huweza kuwasiliana na kutafsiri taarifa mbalimbali za kimwili na kisha mwili hutoa mwitiko baada ya tafsiri.

Machozi yatokanayo na kuhuzunika
(emotion tears) huwa yanaambatana na uso kubadilika kuwa mwekundu, misuli ya uso kukunjika, kutetemeka, pumzi kukatika na mwisho huenda mwili mzima ukakamaa.

Machozi yatokanayo na hali hii ni tofauti ukilinganisha na machozi ya kawaida ya kulainisha jicho, machozi ya hisia huwa na vichocheo aina ya prolactini na adrenocotrico.
Hali hii hudhibitiwa na mfumo usio wa hiyari ‘autonomic system.’

Mfumo huu umepenyeza mishipa ya fahamu inayoshusha mihemko ya kimwili (parasympathetic system) katika tezi inayohifadhi machozi kitaalamu inaitwa lacrimal.
Kemikali maalumu ziitwazo
‘acetylcholine’ hupitisha taarifa za mfumo wa fahamu, kwenda katika vipokezi vilivyopo katika tezi ya lacrimal iliyopo katika kona ya jicho.
Hapo tezi hiyo hupata mihemko na kumwaga machozi kutokana na taarifa ilivyotafsiriwa katika ubongo kam vile hasira au mtu kuudhiwa.

Mawasiliano
Wataalamu wengine wanasema kuwa kulia au machozi ya hisia ni nyanja ya mawasiliano. Kabla watoto hawajaweza kuzungumza hulia.

Hii ndiyo njia pekee kwa watoto wachanga kueleza hisia zao za maumivu, kuumwa au woga.
Hata hivyo watu wazima hulia ili kujenga ukaribu na wenzao. Kulia kwa uchungu kunasaidia walio karibu nao kuonyesha ukaribu wao na upendo kwako.

Wengine wanadai kuwa kulia husaidia kuondoa kiwango cha sumu mwilini.
Mwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Modesta Kimonga anasema kibaolojia mtu hulia kwa sababu ya vichocheo ambavyo husimamia uamuzi.

“Kwa kawaida ubongo wa mtu hupeleka taarifa kuwa mtu anataka kulia kutokana na vichocheo vya lanchrimal” anasema Kimonga
Kimonga anasema tofauti ya kulia kati ya wanawake na wanaume husababishwa na mguso wa moyo.

Wanaume hulia kwa kiwango kidogo kwa sababu wana mguso wa chini tofauti na wanawake.
Mwanasayansi wa
Dutch, Ad Vingerhoets ambaye ametumia miaka 20 kutafiti kwa nini na wakati gani binadamu hulia anasema machozi yanamaanisha kukosa msaada.

Vingerhoets anasema kulia ni maelezo ya hisia kwa watu wazima na ni mawasiliano.
“Watu wengine hulia ili wapate ukaribu, wabembelezwe na watengeneze uhusiano,” anasema
Vingerhoets

Mwanahistoria wa tamaduni, Thomas Dixon anasema machozi wakati mwingine husababishwa na furaha kuliko hasira au huzuni.
“Kwa mfano mwanariadha aliyeshinda medali ya dhahabu, mwanamuziki aliyepata tuzo anaweza kulia kwa furaha,” anasema

Aina za kulia

Dk Mkumbo anasema watu wametofautiana kiwango cha kulia.
“Wapo ambao hulia hata kama wakicheka, lakini wengine ni vigumu kutoa machozi hata wakumbwe na huzuni kiasi gani” anasema
Anasema kulia kunatofautiana kulingana na kiwango cha hisia, mila, tamaduni na maadili.
“Zipo mila ambazo mwanamume haruhusiwi kulia kwani kulia kunafananishwa na woga. Wanaume wa makabila haya hurudisha machozi ndani na kubeba huzuni kwa namna nyingine” anasema Dk Mkumbo.

Kasoro za vilio
Upo ugonjwa kwa kitaalamu unajulikana kama
Bell’s palsy Kupooza kwa uso kupinda mdomo ambapo neva za uso husababisha mtu kutokwa machozi pindi anapokula.
‘Cri du chat’, ambapo kichanga anaweza kulia sawa sawa na paka. Tatizo hili huhusishwa na mfumo wa fahamu.

Wapo wanaolia lakini machozi hayatoki, huu ni ugonjwa.
Wengine hushindwa kutofautisha matukio ya kulia au kucheka na wakati mwingine yote kwa pamoja.
Ukiwa na Swali lolote unawea kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

640px-Bellspalsy.JPG

Ugonjwa wa (Bell’s palsy) Kupooza kwa uso kupinda mdomo
Wabheja sana/wakora weitu/asante sana kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom