Kumbe Maisha siyo magumu!

Kumbe Maisha siyo magumu!

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Nilivyomaliza chuo mwaka jana nilisambaza CV org nyingi na baadhi wakanialika kwa usaili. Nilifanya interview kama 5 bila kupata kazi nikagundua kwamba napoteza vijipesa vyangu kwenye safari zisizoonyesha kuzaa matunda kwa sababu unakuta gharama ya interview moja nauli kwenda na kurudi, chakula na malazi ni zaidi 100,000.

Msimu wa kilimo ulivyofika nikaamua kuachana na kuhudhuria interviews, nikajikita kwenye kilimo. Nililima ekari 6, yaani tatu za mahindi na tatu za alizeti. Mazao yamekomaa na yanaridhisha kwa kweli na makadirio ya chini ya mavuno ni gunia 45 za mahindi na gunia 12 za alizeti.

Kwa maoni yangu mimi hali siyo mbaya kwani mwaka huu haya mazao niliyolima yana bei nzuri sana sokoni. ni mwanzo tu kwani Mwakani nitalima ekari 10. Siyo lazima wote tuwe billionaires anyway ila umasikini lazima ung'oe nanga.

Vijana wa mjini haswa graduates, ingieni shambani mjaribu bahati yenu . Nawakumbusha tu kwamba maisha ni leo na siyo kesho, umri haukusubiri hadi upate kazi za ofisini. Nawakumbusha pia kwamba kilimo cha kutegemea mvua ni kamari
 
Kilimo sahihi ni kilimo cha kumwagilia, ila hiki cha kutegemea mvua hakina uhakika Sanaa! Kinaweza kukutoa mwaka huu, na mwaka ujao kikakuangusha kifo cha Mende!!
 
Kilimo sahihi ni kilimo cha kumwagilia, ila hiki cha kutegemea mvua hakina uhakika Sanaa! Kinaweza kukutoa mwaka huu, na mwaka ujao kikakuangusha kifo cha Mende!!
Uko sahihi 100%
 
Back
Top Bottom