Kumbe Maisha siyo magumu!

Kumbe Maisha siyo magumu!

Nilivyomaliza chuo mwaka jana nilisambaza CV org nyingi na baadhi wakanialika kwa usaili. Nilifanya interview kama 5 bila kupata kazi nikagundua kwamba napoteza vijipesa vyangu kwenye safari zisizoonyesha kuzaa matunda kwa sababu unakuta gharama ya interview moja nauli kwenda na kurudi, chakula na malazi ni zaidi 100,000.

Msimu wa kilimo ulivyofika nikaamua kuachana na kuhudhuria interviews, nikajikita kwenye kilimo. Nililima ekari 6, yaani tatu za mahindi na tatu za alizeti. Mazao yamekomaa na yanaridhisha kwa kweli na makadirio ya chini ya mavuno ni gunia 45 za mahindi na gunia 12 za alizeti.

Kwa maoni yangu mimi hali siyo mbaya kwani mwaka huu haya mazao niliyolima yana bei nzuri sana sokoni. ni mwanzo tu kwani Mwakani nitalima ekari 10. Siyo lazima wote tuwe billionaires anyway ila umasikini lazima ung'oe nanga.

Vijana wa mjini haswa graduates, ingieni shambani mjaribu bahati yenu . Nawakumbusha tu kwamba maisha ni leo na siyo kesho, umri haukusubiri hadi upate kazi za ofisini. Nawakumbusha pia kwamba kilimo cha kutegemea mvua ni kamari
Safi sanaa mkuu
Hongera
 
Hizo ekali sita nitapewa Bure pamoja na mtaji wa kilimo? +lack of capital ni key point tangu jiografia ya form wani tunaisoma
 
Unategemea kupata faida kiasi gani, baada ya kutoa gharama?
Natarajia net profit iwe1.6m. sikutumia gharama kubwa kwani shamba ni la nyumbani na ekari tatu nilipalilia mwenyewe kwahiyo hapo ni gharama za trekta , kuotesha na palizi ya ekari tatu tu. Huku hatutumii mbolea za kununua
 
Mazao yamekomaa na yanaridhisha kwa kweli na makadirio ya chini ya mavuno ni gunia 45 za mahindi na gunia 12 za alizeti
Mavuno kidogo tu ushaanza kuwa motivesheni sipika....

Mkuu safari bado,,, Zungumza hayo ukiwa tayari na hela mkononi...
 
Back
Top Bottom