Kumbe manara hakua pekee yake?

Kumbe manara hakua pekee yake?

Sitetei usaliti, ila kwenye nafasi za ki professional, tusiweke mambo haya ya ushabiki.

Najua nature ya timu hizi imekuwa inafanya hata wachezaji kuhama kutoka Simba kwenda Yanga au Yanga kwenda Simba kuwa ngumu, ila imeshafanyika kuanzia enzi za kina Hamis Gaga, Zamoyoni Mogella hadi kipindi hiki cha kina Morrison, Manara na Senzo.

Kumzuia mtu asiajiriwe timu eti kwa kuwa ni toka utotoni alikuwa mshabiki wa timu fulani au alikuwa mwajiriwa wa timu fulani ni sawa na kutegemea tume huru ya uchaguzi ambayo inahusisha watu ambao hawajawahi kuwa wanachama au wapenzi wa chama chochote cha siasa. Hilo jambo halipo au litachukua muda mrefu sana kuwezekana. Muhimu ni hao watu kutojihusisha na rushwa au hila zozote katika utendaji wa majukumu yao.

Utani wa jadi wa Simba na Yanga unabadilika sana, hasa kipindi hiki ambacho timu hizi zinaanza kuendeshwa kisasa, hili nimelisema sana. Nitakuja na uzi kulielezea hili.
 
Back
Top Bottom