Kumbe mgomo wa wafanyabiashara umefika mpaka Katoro!

Kumbe mgomo wa wafanyabiashara umefika mpaka Katoro!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nilifikiri utaishia Dar Es Salaam na Mwanza. Lakini imekuwa tofauti na nilivyofikiri.

Nikiwa natokea mkoa fulani, leo saa nne Asubuhi, nimepitia Kariakoo Katoro mkoani Geita kwa lengo la kununua vifaa fulani. Sijafanikiwa. Maduka yote yamefungwa. Hiyo ni wazi kuwa nao wamegoma.

Hali haipaswi kuwa hivi. Wengi wanaathirika, ikiwa ni pamoja na Serikali kukosa mapato.

Wahusika wachukue hatua za haraka kungali mapema. Vinginevyo, mgomo unaweza ukaenea nchi nzima.
 
Mbona mi nipo njia panda inyala sjaona huo mgomo ,ila kwa kuwa bila picha uzi haujakamilika ngoja niende mwenyewe,hapo maeneo ya kariakoo na CCm nitupie picha uzi uwe kamili.
 
Leo asubuh nimewafikiria wafanyabiashara wa katoro nikahis watakuwa wanapga hela Sana wakat huu wa mgomo,kumbe nao wapo kwenye mgomo
Njia zote za kuingilia kwenye maduka yaliyopo ndani ya soko la Kariakoo Katoro zimepigwa kamba nyekundu, na yale yaliyopo pembezoni mwa barabara nayo yamefungwa.
 
Wateule na rais mwenyewe wameamua kuupotezea huu mgomo sijajua wanafikiria nini?

Au ndiyo kuwa chura kiziwi maana haisikii ni kama hakuna kinachoendelea nchini
 
We hadi huko mabonde kwinama bk wamefunga maduka kiufupi hii ni nchi nzima kariakoo yenyewe bado wanafungua kwa kutegeana nimekereka kweli na nilikuwa na shida wiki hii
 
Back
Top Bottom