Kumbe mzee Mwinyi "Mzee Ruksa" ni mzaliwa wa Mkuranga, Pwani...

Kumbe mzee Mwinyi "Mzee Ruksa" ni mzaliwa wa Mkuranga, Pwani...

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi maarufu kwa jina la ‘Mzee Ruksa’ leo anatimiza miaka 90. Bado ana nguvu, mchangamfu, mcheshi na anapopata fursa, anawafundisha Watanzania matumizi ya Kiswahili Sanifu na kutoa ushauri juu ya umuhimu wa elimu na kuishi kwa amani na ushirikiano bila ubaguzi kwa misingi ya dini na ukabila.

Alhaj Mwinyi aliyeingia madarakani kuiongoza Tanzania Novemba 5, 1985, alizaliwa Mei 8, 1925 huko Kivule wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, tarehe ya kuzaliwa kwake ina utata kutokana na baadhi ya kumbukumbu kuonyesha kuwa alizaliwa Mei 8, huku tovuti rasmi ya Ikulu ikionyesha kwamba alizaliwa Mei 5.

Elimu

Alhaj Mwinyi alianza safari yake kielimu huko visiwani Zanzibar ambako alisoma katika Shule ya Msingi Mangapwani mwaka 1933 hadi 1936. Baadaye alijiunga na Sekondari ya Dole mwaka 1937 hadi 1942, kisha alijiunga na Chuo Cha Ualimu Zanzibar mwaka 1943 hadi 1944.

Baada ya kuhitimu ualimu kati ya mwaka 1945 hadi 1950 alirudi Mangapwani safari hii siyo kusoma, bali kufundisha. Mwaka 1950 alipandishwa cheo akawa Mwalimu Mkuu katika shule hiyo hadi mwaka 1954.

Mwinyi hakuwa mtu wa kuridhika na elimu aliyonayo hivyo, akiwa kazini, alikuwa akijiongezea elimu kwa njia ya posta na kuhitimu ‘General Certificate in Education’ (GCE). Pia, alisoma kwa njia ya posta na kuhitimu Stashahada ya Ualimu katika Taasisi ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Durban, Uingereza.

Mwaka 1956 Mwinyi aliajiriwa kuwa mkufunzi katika Chuo Cha Ualimu Zanzibar kazi aliyoifanya hadi mwaka 1961. Baadaye alijiunga tena na Taasisi ya Regent ya London, Uingereza ambako alisoma kwa njia ya posta na kuhitimu cheti cha ufundishaji Lugha ya Kiingereza.

Mwaka huohuo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Hall, Uingereza na kusomea kozi ya ufundishaji (Tutors’ Attachment Course) hadi mwaka 1962. Mwinyi pia ana cheti ya Lugha ya Kiarabu alichokipata kwa kusoma Cairo, Misri kati ya mwaka 1972 na 1974.

Kwa hiyo, Mwinyi ni mwalimu aliyekamilika. Alipojitosa katika siasa na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi, ni kama alikuwa amebadilisha darasa kutoka lile lenye kuta ambalo huwa na wanafunzi kati ya 24 na 45, wakati ule, hadi nchi nzima kuwa darasa na wananchi kugeuka kuwa wanafunzi.

Kazi na siasa

Mwaka 1964, akiwa na umri wa miaka 39, Mwinyi alianza rasmi harakati za kisiasa; alijiunga na Chama cha Afro Shiraz (ASP) huko Zanzibar. Umahiri wake katika kujenga hoja, ushawishi wake na mvuto kisiasa vilimwezesha kukitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Kati ya mwaka 1964 na 1965 alishika wadhifa wa katibu mkuu wa muda katika Wizara ya Elimu kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Biashara Zanzibar – Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC), mwaka 1965 hadi 1970.

Ndani ya chama, kati ya 1966 na 1970 alikuwa mweka hazina msaidizi katika Tawi la ASP la Makadara, Zanzibar. Vilevile, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) kati mwaka 1964 na 1977.

Majukumu mengine aliyowahi kushika Alhaj Mwinyi ni ujumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Chakula na Lishe na Mwenyekiti wa Zanzibar Censorship Board (1964-1965).

Aidha, Alhaji Mwinyi amewahi kuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1972 – 1975), Waziri wa Mambo ya Ndani (1975 – 1976). Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri hadi mwaka 1982 aliporejea nyumbani mwaka huo aliteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na mwaka 1983 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Kuingia Ikulu

Mwaka 1984, hali ya hewa ya kisiasa ilipochafuka Zanzibar kutokana na hatua ya Alhaj Aboud Jumbe kubanwa kuhusu hoja aliyoibeba binafsi kutaka mfumo wa Muungano wa Serikali mbili ubadilishwe, Mwinyi alichaguliwa kurithi nafasi hiyo akiwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Agosti 1984, alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini uongozi wake thabiti, upeo mkubwa na maono aliyokuwa nayo, mwaka 1985 alipendekezwa na CCM kuwa mgombea urais na kwa vile enzi zile zilikuwa za mfumo wa chama kimoja, hakuwa na mpinzani, akachaguliwa kuwa Rais wa Pili wa Tanzania akichukua mikoba ya Rais wa Kwanza wa Tanzania ,Mwalimu Julius Nyerere aliyeamua kung’atuka.

Katika maisha ya kawaida, Mwinyi ni mpenda michezo na mara nyingi hushiriki ‘jogging,’ matembezi ya kuchangisha fedha na kufanya mazoezi mepesi ili kujiweka vyema kiafya.

Mzee Ruksa ana wake wawili; Sitti na Khadija na ana watoto na wajukuu kadhaa. Mmoja wa watoto wake ni Dk Hussein Mwinyi ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mambo aliyofanya

Alhaj Mwinyi alirithi nchi yenye uchumi ulioharibika kutokana na kutokana na ugumu uliokuwapo, aliamua kufanya mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na nchi wahisani ili kufufu uchumi.

Halafu aliandaa Azimio la Zanzibar lililolegeza masharti na miiko ya uongozi iliyokuwamo katika Azimio la Arusha. Kwa hatua hiyo, akafungua madirisha ya soko huria na wananchi wakaanza kuagiza na kupata bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Kwa kuzingatia Azimio la Zanzibar, ikawa ruksa kwa viongozi kuwa wakurugenzi katika mashirika binafsi, kuwa na hisa, kumiliki mali. Hii ilikuwa na maana kwamba sera ya Ujamaa ya CCM ilitupwa kapuni – mashirika ya umma na viwanda vya umma vikaanza kuuzwa kwa kisingizio cha ubinafsishaji.


Baada ya kibano kutoka mashirika ya fedha na nchi wahisani, Serikali ya Mwinyi aliamua rasmi kurejesha mfumo wa vyama vingi, lakini ilitumia mfumo wa kisheria ikaandaa Waraka wa Serikali Namba Moja (White Paper) ambao wananchi waliulizwa kama wanataka mfumo wa chama kimoja au vyama vingi. Asilimia 80 ya watu ilisema inataka chama kimoja, lakini kwa ushawishi wa Mwalimu Nyerere, Serikali iliridhia hoja za waliosema wanataka mfumo wa vyama vingi ili kufungua milango ya wengi kushiriki siasa.

Vyombo vya habari binafsi viliruhusiwa; magazeti, majarida, redio na televisheni viliruhusiwa ili kuwapa wananchi uhuru wa kupata habari. Kwa hiyo, uwazi ulianza kushamiri.

Kadhalika, Mwinyi alianzisha utaratibu wa wizara kueleza zimefanya nini katika kipindi cha mwaka mmoja japokuwa utaratibu huo haukuendelea. Ili kuhakikisha unakuwapo uwajibikaji wa hali ya juu kwa wafanyakazi, katika mwaka wake wa kwanza wa uongozi, alikabidhiwa fagio la chuma ili kuwaondoa wafanyakazi wote wasiowajibika serikalini.

Mwinyi ndiye aliyetuliza pepo mbaya alipotaka kulivamia Taifa baada ya waumini wa Kiislamu kuvamia na kuvunja mabucha ya nguruwe eneo la Manzese, Dar es Salaam.

Aliwaambia waumini hao Tanzania ni nchi inayoamini katika uhuru wa kuabudu hivyo anayetaka kula nguruwe ruksa.

Vilevile, Mwinyi ndiye aliyetuliza pepo mwingine mbaya pale waumini wa dini ya Kiislamu Zanzibar walipoandamana kupinga kauli ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Kawawa (marehemu) aliyedai ndoa za wake wengi zinachangia maambukizi ya Ukimwi. Mwinyi aliwaambia yale yalikuwa maoni yake na si msimamo wa Serikali.

Mwinyi atakumbukwa na wafanyabiashara ndogondogo kwa vile ndiye aliyeruhusu kila mtu kufanya kazi halali ya kumwingizia kipato. Mazingira hayo kwamba ni ruksa kufanya kazi yote halali ndiyo yalisababisha Watanzania kumbatiza jina la ‘Mzee Ruksa’.

Mbali ya kuhimiza umuhimu wa elimu, alielimisha matumizi ya kondomu ili kujiepusha na maambukizi ya ukimwi. Hata hivyo, mwaka 2009 alipohutubia Baraza la Maulid na kuwataka Waislamu wajikinge na maradhi hayo, kijana mmoja alimpiga kibao.

Hadi leo akipata fursa au akialikwa kwenye vipindi mbalimbali hufafanua matumizi sahihi ya maneno au mnyambuliko sahihi. Mfano ni maneno “onya” na “ona”. Anafundisha kitendo cha kutaka mtu aone kitu fulani unasema “onesha” na siyo “onyesha” kama ilivyozoeleka kwani onyesha linatokana na onya.

Anapozungumza, hadi leo, hotuba yake hujaa methali na nahau au tamathali nyingine za semi na lafudhi inayoburudisha wasikilizaji. Huyo ndiye Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Ruksa ambaye kwa sasa anaishi Msasani, Dar es Salaam.

Huyu ndiye mzee Ruksa amabay ni mzaliwa wa mkuranga , Pwania ambaye sasa kagonga miaka 90 net. Allah ampe maisha mema na yenye afya tele.




IMG_3814.JPG


tumblr_mx15dy2fcT1t2e1lvo1_500.jpg

Ali%20Hassan%20Mwinyi.jpg


5..jpg

mj-na-rais-mwinyi.jpg
IMG_5624.JPG

AWOEKO.jpg
405630859.JPG
unnamed%2B%2855%29.jpg

pg1_.jpg
Mwinyi+Nyerere.jpg
wasira_clip.jpg
 
Hukujua wakati Husein Mwinyi Dr, aliwahi kuwa mbunge wa kuchaguliwa mkuranga??? kwa misingi hiyo hiyo
 
Hongera Mzee japo kuna watu watakuja kukupongeza ilhali wakiponda Azimio la Zanzibari kwani wao wanashikilia Azimio La Arusha kwa maneno na kwa Vitendo wanaliishi Azimio La Zanzibari, na sasa wamefuata nyayo za wakubwa wao kwa kuanzisha tawi jingine eti wanasema ni wazalendo kwa vile wanaliishi Azimio la Arusha kwa Maneno na Wanaliishi Azimio La Zanzibar uliloliasisi kwa vitendo vyao
 
Hata mzee Aboud Jumbe ni wa mrima,hapa ni kuonesha kuwa ule msemo wa " watu wa bara hawaajiriwi zanzibar " ni uongo, wanaajiriwa na wanamiliki ardhi, ukienda kwenye vikosi vyao wamo kibao....wengine hata jeshi/polisi huandikisha kule (wenye jamaa zao) .
 
Picha zote nimeziangalia vizuri, hiyo ya mwisho hiyo imenifanya nicheke ghafla, sasa hapo nani ananyoshewa kidogo?
 
Tutakukumbuka kwa kufanya biashara akiwa Ikulu na kuruhusu biashara ya magendo. Aliaribu masharti na maadili ya viongozi.
 
hahahaha, JF kiboko, ........picha ya mwisho, loh, vituko JF havitoisha
 
Picha zote nimeziangalia vizuri, hiyo ya mwisho hiyo imenifanya nicheke ghafla, sasa hapo nani ananyoshewa kidogo?

huyo ndo amiri jeshi ajae,hamna lelema,bhita ni bhita mura.......
 
Vilevile, Mwinyi ndiye aliyetuliza pepo mwingine mbaya pale waumini wa dini ya Kiislamu Zanzibar walipoandamana kupinga kauli ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Kawawa (marehemu) aliyedai ndoa za wake wengi zinachangia maambukizi ya Ukimwi. Mwinyi aliwaambia yale yalikuwa maoni yake na si msimamo wa SeriKali
Kwanini katika aya hii umekusudia kuongopa? Au kwa kuwa Tanganyika kulikuwa na RTD tu wakati huo hivyo ukakosa kujua kwa usahihi nini kilifanya waislam kule Unguja tuandamane?

Sofia Simba alikuwa akizungumzia juu ya haki sawa kwa mwanamke kwamba kitendo cha kitabu cha waislam kutoa uhuru kwa wanaume kuoa wake wengi ni uonevu kwa wanawake hivyo naye atawasilisha hoja ili wanawake nao waruhusiwe kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja ndipo haki sawa kwa mwanamke itakuwa itatendeka. Na hivyo hitimisho la hoja yake ni kitabu cha waislam kibadilishwe au serikali iweke sheria au itambue pia ndoa ya wanaume wengi!

Ni hayo tu, mengine nimeona "kiasi yanaridhisha" hivyo no comment
 
Mzanzibari ambae si Mzanzibara aliyewahi kuwa Maarufu saa kwenye siasa za Zanzibar toka kabla na baada ya mapinduzi ni mmoja tu!

Anaitwa Thabit Kombo na baba'ke aliwahi kuwa na Masuria wawili (watumwa wawili wa kike).

Unajuwa Washirazi ni akina nani? Ndiyo hao leo hii mnawaita Wabulushi, Rostam mmoja wao.
 
rais ws Zanzibar ambaye ni mzawa hasa wa zenji ni huyu shein engine wote ni wabara ukianzia karume asili yake songea... komandoo asili yake tabora....
 
Back
Top Bottom