Pre GE2025 Kumbe Nape na Makamba ni trailer tu, lengo hasa ni waleee!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Ili umpe kipigo cha mbwa koko mtoto wa kambo pasipo lawama, basi anza kwa kumfinya mwanao wa kumzaa. Anapoanza kulia mtoto pendwa ndipo unanza kushusha kipondo cha kuvunja mikono kwa mtoto wa kambo.

Majirani wanaotazama kinachoendelea watajua unagawa adhabu kwa wote bila upendeleo, lkn kumbe umedhamiria kumtia ulemavu mtoto wa kambo.

Pia soma: Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Nape na Makamba wamefinywa tu, ili sasa watoto wa kambo (wale wa kanda ilee) waanze kushughulikiwa ipasavyo, na hakuna atakayestukia. Itaonekana ni mpango wa kawaida wa mama.

Inadaiwa watoto hawa hawaishi lawama, wanadai wanabaguliwa, wanafanya mipango hatarishi ya kuandaa mtu wao wa kumtoa mama ndani ya nyumba. Mama kaona ili kushughulika nao pasipo lawama, acha awafinye wanaye wa kuzaa, waanze kulia ndipo awageukie watoto wa kambo.

Ndiyo maana tetesi zinasema haya yaliyofanyika ni tone tu la mabadiliko makubwa yanayokuja. Watoto wa kambo wajiandaye kisaikolojia.
 
Weka na majina wenzio hua wanafanya HIVYO
 
Mmeshashutukiwa.

Mmemjaza uwongo na kumtisha tisha chapa chapa dengu, kumbe yote yale ni kufunika hujuma zenu za Uasi.

Sasa bosi wenu aliyekuwa anawakingia kifua....kapigwa pwaaa...chiini ...Mama wa ndani keshawahtukia.

Ni hivi, hakuna cha watoto wa kambo wala nini, hii ni nyumba yetu, mbuzi zetu na urefu wa kamba zake!

Hata mjaribu vipi kututenganisha, ndio kwanza tuna shikamana haswa.

Tanzania haijaitwa Bongo hivi hivi tu.
 
Hivi mna uhakika kiasi gani mnavyoshadadia wao kutolewa hawa matajiri kwamba ndo mwisho??

Kesho wakirudishwa sehemu nyeti zaidi hiyo aibu mnaweka wapi!!

Hizi siasa za Tanzania hamjazizoea mpk tu??

Punguzeni wenge kigodo hata wake zenu hawako ivo😂
 
Aassh kumbe lengo lake ni kusafisha Sukuma Gang! Sasa nimeanza kumuelewa Chifu Hangaya.
 
Wewe ni mmoja wa hao watoto wa kambo waliozungumziwa humu?
 
Mimi hadi britanicca akisema ndio nitaamini ,maana wewe bado unaweweseka kwa kutolewa wapendwa wako, bado huamini wala kukubali kilichotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…