Kumbe ndio maana hamuolewi!!!

Kumbe ndio maana hamuolewi!!!

mi nadhani sababu kubwa ya kuchelewa kuoa au kuolewa ni; matatizo mengi yanayoongelewa ktk ndoa. Wanandoa wengi pamoja na wazazi wamekua wakiwaambia vijana na watoto wao kuwa ndoa ni ngumu na ina shida na matatizo mengi. Hii imepelekea vijana wengi kuchelewa kuoa au kuolewa wakidai hawataki kuingia ktk shida mapema. Huo ndo mtazamo wangu.
Na hivi vimisemo navyo huchangia sana.... Mara ndoa ndoana..................Mara mdoa msalaba...............Mara mbingu za maisha.............. mara ndoa kuvumiliana wakati hicho cha kuvumiliwa hakitajwi ila huwa kinasemwa kijumla...shida.........
 
Kuna msemo mmoja wa Waingereza usemao......."Ya nini ufuge ng'ombe wakati maziwa yanapatikana tu kiurahisi?"
 
kuoa ni wito wanaume wenyewe huo wito hawana
Tatizo lenu mpaka mdanganywe......... We mimi nataka ngono ya leo au kesho...nikija straight kwamba nataka kwa muda tu.... sipati kitu unadhani nitakwambia nini wakati najuwa ukitajiwa kuolewa unaachia mzigo..?? Na lingine ni kuwa waowaji tukija straight bila chenga kukueleza kuwa nataka nikuowe huwa mnatuona wazugaji..............sasa tufanyeje..??
 
Siku hizi wanaume hupata mapenzi kirahisi sana kutoka kwa wanawake kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hata ukiongea na mzee mwenzangu Bishanga atakubaliana na mimi.

Zamani enzi zetu makahaba walikuwa ni wachache sana na ilikuwa ni aibu sana kwa mwanaume kwenda kwa kahaba. Ni wale tu waliokata tamaa ndio ambao walikuwa wanakwenda kwa makahaba.

Enzi zetu sisi, mipaka na kanuni za jamii katika kushiriki mapenzi kabla ya ndoa zilikuwa ngumu sana. Mwanaume analazimika kuoa haraka kwa sababu kupata ridhiko nje ya ndoa ilikuwa ni shughuli pevu, na ndio maana wastani wa umri wa kuoa wakati huo ilikuwa ni kati ya miaka 23 mpaka 25, tofauti na siku hizi umri wa kijana kuoa umefikia miaka 30 mpaka 35. Mpaka hapo unaweza kuona ni kwa namna gani wanaume wanachelewa kuoa.

Leo hii inaonekana kama vile kila msichana ni kahaba. Hata wale watoto wanaoitwa, ‘watoto wa geti kali,’ wanapatia mimba humo humo ndani ya mageti, sema tu kwamba, wengi huzichoropoa kiurahisi. Kufanya mapenzi ya utotoni hivi sasa ni kama sifa. Wataalamu wanasema kwamba, watoto wa kike wanaotoka kwenye familia zenye vurugu na tafrani hushiriki mapema tendo la ndoa.

Hebu tujiulize, je ni familia ngapi zina amani? Kwa hiyo watoto wa kike wengi huanza mapenzi utotoni na hivyo, vijana hupata ‘asusa’ kwa kadiri wapendavyo, ni rahisi sana. Na ndio maana wanachelewa kuoa kwa sababu kile ambacho (kujamiiana) wanaamini ndio sababu ya wao kuoa wanakipata kwa urahisi.

Ngoja ninywe chai nikirudi hapa nakupa fact za akili za wanaume wa kisasa ni zaiidi ya UHARO wa KIPINDUPINDU. Stay tuned!
 
enzi zenu kulikuwa hakuna watoto nje ya ndoa?
Ni kweli maadili yameshuka, lakini umefikiria hali ya maisha ya sasa na ya zamani? Maisha magumu mwanaume hakurupuki kwenda kuoa hadi ajipange. Tofauti na 'enzi zenu' za riziki huletwa na Mungu.

Hizo enzi zenu wanaume walikuwa wanajiamini,wana uthubutu wa kupambana na maisha tofauti na wanaume wa enzi zetu hz vijana wa kiume wanataka kulelewa, mariooo. .

Enzi zenu heshima ya mwanamke inapimwa kwa ndoa. Enzi zetu heshema ya mwanamke/mwanaume inapimwa na tabia. Regardless ameoa/ameolewa au hajaoa/hajaolewa.

Hebu waacheni wanawake wapumue. Kha!
Hapo kwenye BOLD ............. Watoto wa nje walikuwepo sana tuuuu na ndiyo maana ikatafutwa namna ya kuhalalishwa hali hiyo.......... KITANDA HAKIZAI HARAMU............. Tehe.tehe.teeeeeeeee
 
Duh!Mawe yamempata ndege mahali pake haswaa!
 
Mtambuzi siye hatuko hivyo, unatusingizia tu bure.
 
Tatizo lenu mpaka mdanganywe......... We mimi nataka ngono ya leo au kesho...nikija straight kwamba nataka kwa muda tu.... sipati kitu unadhani nitakwambia nini wakati najuwa ukitajiwa kuolewa unaachia mzigo..?? Na lingine ni kuwa waowaji tukija straight bila chenga kukueleza kuwa nataka nikuowe huwa mnatuona wazugaji..............sasa tufanyeje..??
hili neno mkuu
tatizo upande wa pili wanapenda kuambiwa wananachotaka kusikia
 
Kimpango wangu naliona hili kama ifuatavyo:-

1. it seems ni kweli idadi ya wasichana waliotayari kuolewa ni kubwa kuliko ya wavulana,ukichunguza kwa makini wasichana wa miongo hii wanawahi sana kukua kuliko wavulana na hili limesababisha ya kwamba muda ukifika wa kuji-ndoa msichana akimpata mvulana (bf) faster anawahisha mimba ili iwe gear ya kuforce ndoa ndio maana wanandoa wengi wana mtoto tayari wakiwa harusini.

2. Kuna hii idea ya kula shule mpaka basi nayo imekuwa noma kwa upande wa wasichana,vile marks zenu zipo chini mnasoma na kusoma na hamu juu ya kuendelea kusoma hatma yake wanakosa wenye viwango ama kukimbiwa na wanaume pale wanapo-settle kuanza maisha baada ya kumaliza shule kati ya wanaume 10 wenye real interest 3 hapo issue tena.

3.Kwa kweli tumekuwa na tabia chafu sana sana si wanaume sime times na kuwaogopesha wasichana kiasi cha kuwafanya akina dada kutokusikia habari za ndoa na kuamua kuwa na mtoto wake wa deal(bila kuolewa) na life linasogea nali-support sana hili life is too short.

4. Hali ya maisha ya wasichana iko pouwa kuliko wanaume kwa asilimia kubwa na hili linatokana na kazi,backup za ndugu jamaa na marafiki maana wanaamini binti hatakiwi kupata shida mwisho wa siku binti hutoka pouwa na anataka kutoka na mwanaume aliye pouwa hii "selection" inakuja kuwa sumu kwani kupata type hii ni issue hapa mjini na mwishowe huishia kutoka na wapita njia walio chini wakijua unashida na hawana mpango wa kutengeneza maisha nawe kwani sio class yao.

Nwkl.
 
wakuu nielewesheni, pengine sija scroll sana humu jf. hivi sredi inapowekewa nyota kwa mbele ina maanisha nini. Hata hii kamba imewekewa nyota hizo. nijulisheni jamani
 
pole shem wangu ashad.... Naona kimeumana

Umepotea kiaina Shem, ingepita 2 more days ilikua nikutafte bana sio kawa... Yameumana bana Mtambuzi katushadadia mno.

Ahsante Da AshaDii kwa angalizo, ushauri wako nimeupokea tena kwa mikono miwili..........................

Afadhali bana, naomba ujitahidi uwe unabalance kidogo pande zoote...

hujambo Asha?
Wala usikonde,naandaa uzi ...title...'Mianaume ndivyo tulivyo'...stay tuned!

B' Mie mzima wa afya kabisa... Lete hio topic bana, tuwaponde roho zetu zifurahi....lol... (hata kama twawahitaji...

Mtambuzi nashukuru MUNGU kwa kuwa unaendelea vizuri umeweza hata
kuendelea na tungo zako zenye mlengo wa kike.
kwa watoto bana, hawa watoto wenu wa mageti makali ndo wanakuwaga vicheche sana huko mbele i.e. elimu ya juu, vyuoni,
kwa kuchelewa kuoa ni kutokana na watu kuogopa majukumu, si wamezoea kulelewa na wazazi,
la kutongoza wanaume nataka niwaulize
hawa binti zangu akina bebii, feisibuku, ashadi, kongosho na wengineo kibao
eti hii tabia ya kutongoza wanaume mmeipata wapi
?


Auntie mie sina tabia ya kutongoza kabisa... ila tu ninatabia nikimpenda nahakikisha kanifaham, asipovutiwa namimi enough kunitongoza nachapa Lapa! lol (hio ilikua siku nyiiiingi kabla sijaolewa by the way )
 
When a victim is unable to defend against the monster, the only option available is to cry. Mkuu nadhani umesikia kilio chao, hamisha mashambulizi, ila ukileta huku kiumeni, inabidi ujiandae mkuu si unajua we constitute what people say a stronger sex. Unatakiwa nawe uwe strong na roho ngumu na uajsiri kama ule wa kumwagia maji ile kituuuuuuuuu!
 
Umepotea kiaina Shem, ingepita 2 more days ilikua nikutafte bana sio kawa... Yameumana bana Mtambuzi katushadadia mno.



Afadhali bana, naomba ujitahidi uwe unabalance kidogo pande zoote...



B' Mie mzima wa afya kabisa... Lete hio topic bana, tuwaponde roho zetu zifurahi....lol... (hata kama twawahitaji...




Auntie mie sina tabia ya kutongoza kabisa... ila tu ninatabia nikimpenda nahakikisha kanifaham, asipovutiwa namimi enough kunitongoza nachapa Lapa! lol (hio ilikua siku nyiiiingi kabla sijaolewa by the way )

Inaonyesha wewe siyo .com kivile,
lakini wewe ni mjanja,
wadogo zako siyo wajanja kama wewe,
hebu wape siri ya mafanikio yako dada.
 
Auntie mie sina tabia ya kutongoza kabisa... ila tu ninatabia nikimpenda nahakikisha kanifaham, asipovutiwa namimi enough kunitongoza nachapa Lapa! lol (hio ilikua siku nyiiiingi kabla sijaolewa by the way )

AshaDii
Double plus for this!............................nothing like a woman who isnt afraid to go after what she wants!........ in a classy way for that matter!!!
 
Back
Top Bottom