Naomba tu nikushauri kuwa ukitaka kuujua Uislam, soma Quran na fuatilia visa vya mitume, usifate watu wanaojiita ni Waislam kama reference ya Elimu ya Uislam kwani kuna kundi kubwa lisilo kuwa na Elimu ya Kiislam pamoja kujiita ni waislamu na kwa bahati mbaya huwezi kuwatofautisha.
Suala la kumchukulia mzee wa Taarabu kuwa ndiye reference ya Uislam, sio sawa kwani tayari ameonesha udhaifu mkubwa wa kutoa mada na mwishowe kuleta mkanganganyiko.
Kuhusu Nguruwe kama ulivyo ambiwa ni red meat tena ni moja ya Nyama ambayo imekatazwa kutokatana na madhara yake mengi kwa afya ya binadamu...(hilo ni somo tofauti). White meat zinapatikana kwa kuku, samaki nk
Natoa tu angalizo kuwa Quran sio story book ya kusimulia watu ili wafurahie kama mashairi ya Nyimbo nk
Kile ni Kitabu KITAKATIFU hivyo ni vizuri kiheshimiwe na anaye toa hoja kwa kurefer Quran awe na Eimu ya kutosha kuhusu anachotaka kukiongelea!