Ndio, inawezekana. Maana nchi zenyewe ni majirani.
Hata hivyo tafiti nyingi za kisayansi kuhusu Tea (Camellia sinensis) zinaelemea zaidi kwa Uchina kama "origin" of Tea.
Hata hivyo cha muhimu ni kukubali kuwa lugha yoyote lazima itachukua maneno kutoka kwenye lugha zingine. Na haimaanishi kwamba lugha inapokuwa ina maneno ya kuazima basi si ya muhimu, na kwamba labda ile lugha ambayo ndio asili ya maneno mengine ya lugha zingine basi ni bora zaidi. Kwa jamii yetu ya kiTZ pamoja na kwamba lugha yetu ya kiswahili ni changa na ni mchanyato wa lugha zingine, bado ni lugha bora kwa jamii yetu. Kama ambavyo kifilipino ni bora kwa wafilipino kuliko lugha zingine.