- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nmeona hizi taarifa je zina uhalisisa wowote?
- Tunachokijua
- Abdul Nondo ni mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha ACT-wazalendo. Mnamo tarehe 1-12-2024 Nondo alitekwa na watu ambao hawajafahamika katika kituo cha mabasi Magufuli jijini Dar es salaam majira ya saa 11 alfajiri alipokuwa akitokea Kigoma. Taarifa zake zilitolewa na chama chake lakini pia kupitia kwa aliyewahi kuwa kiongozi wa chama hiko Zitto Kabwe na baadaye kutoka kwa taarifa rasmi ya jeshi la polisi.
Usiku wa tarehe 1-12-2024 Nondo alipatikana akiwa ametupwa katika ufukwe wa bahari ya hindi maarufu kama Coco beach Dar es salaam na kisha baadaye kuomba msaada kwa watu ili apelekwe kwenye ofisi yao ya chama iliyopo Magomeni, Dar es salaam. Baadaye alipelekwa katika hospital ya ya Agha Khan kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake kutokuwa nzuri kwa muibu wa chama chake.
Mara baada ya tukio hilo kumekuwepo na kipande cha video kinachowaonesha waandishi wa wa kituo cha Wasafi Fm kwenye kipindi cha Goodmorning huku ikiwa imeambatana na grafiki inayosomeka ‘imebainika nondo kujiteka Mwenyewe’. Tazama hapa
Madai ya Nondo kujiteka Mwenyewe
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kuhusu madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Kipande cha video kilichoweka hakiendani na grafiki inayoeleza kuwa imebainika Nondo ajiteka mwenyewe. Kipande hiko cha video kinawaonesha watangazaji hao wa kipindi cha good morning wakijiuliza baadhi ya maswali kulinga na tukio la kutekwa kwa Nondo. Video hiyo imetokea kwenye kipindi cha good morning kilichofanyika tarehe 2-12-2024.
Jeshi la polisi kupitia taarifa yao waliyoitoa tarehe 02-12-2024 waliandika kuwa Nondo amepatikana na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ni nani aliyefanya kitendo hiko, sababu ilikuwa nini na ili hatua nyingine za kisheria zichukuliwe. Jeshi liliandika;
“Baada ya yeye kupatikana uchunguzi unaendelea ili kuwapata wahusika wa tukio hili ikiwa na sambamba na kupata ukweli wa sababu au chanzo (motive) cha tukio hili ili hatua nyingine za kisheria zichukuliwe’’
Hivyo madai ya kuwa Nondo amejiteka si ya kweli kwani wenye mamlaka ya kutoa taarifa ambao ni jeshi la polisi wameeleza kuwa bado uchunguzi unaendelea, lakini pia maandishi yaliyopo kwenye grafiki hayaendani na kilichokuwa kinasikika kwenye video hiyo.
Madai ya Nondo kutekwa na kikosi cha Red Brigade
Kumekuwapo na taarifa nyingine pia ambayo inaeleza kuwa waliomteka Nondo ni kikosi cha Red brigade cha CHADEMA, taarifa hiyo imbeambatanishwa na picha za taarifa kwa umma iliyotolewa na jeshi la polisi kuhusu wanaodaiwa kutaka kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo. Mathalani mtu mmoja aliandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X kuwa;
Kwa taarifa hii kutoka Jeshi la polisi ni wazi kuwa waliomteka @abdulnondo2 ni kikosi cha Red Brigade cha @ChademaTz.
Soon mambo yote yatawekwa wazi na dunia itajua ujuinga wao
Tazama taarifa hiyo hapa.
Tarehe 4-12-2024 jeshi la polisi limetoa taarifa kwa umma kuhusu kukakamatwa kwa watu waliotaka kumteka Tarimo tarehe 11-11-2024 ambapo wameweka orodha ya majina ya watu hao pia na hakuna mhali katika taarifa hiyo ambapo wameelezea kuhusu suala la kutekwa kwa Nondo wala kuhusu kikosi cha Red Brigade.
JamiiCheck imefuatilia kuhusu uwepo wa kikosi cha Red brigade na kubaini kuwa kikosi hiko kilifutwa mwaka 2019 kwenye marekebisho sheria ya vyama vya siasa, Sura namba 258 iliyofanyiwa Marejeo mwaka 2019 chini ya kifungu cha 8E (1)
Hivyo madai hayo si ya kweli kwani kikosi hiko kilishafutwa, lakini pia kilichoandikwa na jeshi la polisi kwenye taarifa kwa umma wameongelea kuwashikilia waliotaka kumteka Deogratius Tarimo na si kuhusu red brogade ama kutekwa kwa Nondo.