Kumbe nyumba anayoishi Alikiba kapanga!

Kumbe nyumba anayoishi Alikiba kapanga!

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mjengo anaoishi mkali wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua , Ali Saleh Kiba uliopo Kunduchi- Mbezi Beach jijini Dar , unadaiwa kuzua utata mkubwa hivyo kulilazimu kuchimba na kubaini kuwa nyumba hiyo si ya msanii huyo bali amepangisha.

Awali, Kiba alikaririwa akisema kuwa , mjengo huo wa kifahari ni wa ndugu yake aliyepo nje ya nchi ambaye alimpa ili aishi na ndugu zake (wa Kiba ) wakati yeye (mmiliki ) akiwa hayupo.

Siku kadhaa mbele , baada ya Kiba kuvamiwa nyumbani hapo na watu kupora vitu huku akinusurika kuuawa , jamaa huyo alikaririwa redioni na kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa nyumba hiyo ni yake .

Ilidaiwa kwamba , mara tu baada ya Kiba kutangaza kumiliki nyumba hiyo, ilidaiwa kuwa aliibuka mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mariana ikisemekana eti ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo.

Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba , Mariana , akiwa mwandani wa Kiba ndiye aliyemuweka Kiba aishi kwenye nyumba hiyo wakati yeye ( Mariana ) kwa sasa anaishi nchini Singapore barani Asia.

"Ninyi mnasema ule mjengo ni wa Ali (Kiba )? Acheni hizo , kwa taarifa yenu hiyo nyumba kapewa na mrembo f ' lani hivi amazing , anaitwa Mariana , ni Mbongo anayeishi Singapore.

"Muulizeni huyo Kiba awaambie ukweli, " kilisema chanzo chetu kikisisitiza: "Hata Mariana aliposikia eti nyumba ni ya Ali (Kiba ) alishangaa na akamaindi ile mbaya hivyo kwa sasa sidhani kama wanaelewana kwa ajili hiyo."

Baada ya kukutana na mkanganyiko huo , gazeti hili lilimtafuta Kiba ambaye alikiri kwamba kweli nyumba hiyo siyo yake bali amepangisha huku akikana kusema kuwa anaimiliki .

Alipoulizwa juu ya madai ya kupewa nyumba hiyo na mwanamke aitwaye Mariana , Kiba alisema hayo ni maneno tu kwani anachojua yeye amepangisha.

"Kwanza hebu nitumie picha nijue ni nyumba gani ?" aliomba Kiba ambapo alitumiwa picha kwa WhatsApp ndipo akajibu :

"Okey , kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba ."
 

Attachments

  • 1432464836011.jpg
    1432464836011.jpg
    24.4 KB · Views: 3,167
Hapa habari hii ina nia ya kumkumbusha Kiba asijisahau kupita kiasi. Atafute eneo na ajenge nyumba ili apate sehemu ya kupumzika kama msanii mkubwa.

Sitarajii watu wenye akili timamu wakahusisha habari hii na ushindi au na upinzani wa timu.

Mdogo wangu Kiba, anayekupenda siku zote hawezi kukusifia au kukusapoti katika kuteketea. Mawazo hayo yachukulie kwa mtazamo chanya. Wapotezee wanaoonyesha kukusifu wakati wewe unajua kuwa hiyo ni changamoto kwako. Napenda niseme si mara zote maadui zako wawe wale wanaokusema vibaya, bali maadui wakubwa ni wale wanaokusifia katika ujinga.

Jipime kijana, kuna watu wanajitoa akili kukushabikia, nakuthibitishia ukipata maendeleo hao ndo watakuwa maadui zako. Wote wanaokusapoti sasa idadi kubwa walikuwa supporters wa Diamond, baada ya kijana kujitambua wakabadili ID na kuwa hatters. This is how the world it is. Keep it up Kiba na uwe focused, kubali changamoto na uwe tayari kushindana kwa nia ya kupata mafanikio zaidi. Tumia kumi ili upate ishirini na usitumie kumi kwa ajili ya kuharibu kumi ya mwenzako.
 
Ngoja tumtie ujinga yeye na wanaojiita mashabiki wake " hiyo nyumba ni yake Kiba na anazo kama hizo 69 ktk mikoa yote TZ na huyo wanayejifanya wamemuhoji Kiba si Kiba ila ni ktk wale wasiopenda mafanikio yake mutasema poo mwaka huu tumeanza kukachukua kademu chake sijui kidoti halafu tunakuja wema halafu peni tutamaliza na huyo wake wa sasa" munalo hilo limewaganda
 
Kwa sasa tunapiga kura tu kwa kiba. Mambo ya kupanga hayatuhusu. Kwani kupanga ni dhambi? Wasanii wangapi wanapanga. Tuondoleeni upuuzi.
 
Back
Top Bottom