Kumbe P-Funk siye aliyetengeneza mdundo wa She Got a Gwan

Kumbe P-Funk siye aliyetengeneza mdundo wa She Got a Gwan

Beat nyingi mbona hatengenezi Majani, kuna Ludigo Bishota maarufu kama Professa Ludigo kafanya kazi kubwa mno, pia hao wengine wakiwemo.

Ndiyo hivyo ni mmiliki wa studio ndo maana sifa anabeba yeye
Kama huyu LUDIGO alifanya ngoma nyingi sana za wagosi, ila nimejaribu kumtafuta kwenye mitandao nimemkosa kabisa aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwah kusikia interview moja Ngwair alihojiwa nini maana ya she got gwan,akasema kwa jinsi manzi alivyo mzuri bas she has to go on,yaan muache aende tu
Gwan ni neno la kijamaica linalomaanisha 'go on' ila mara nyingi hutumika kwenye sentensi fupi 'wa gwan' kumaanisha 'what is going on'.

Mpaka anafariki dunia, Mangwea hakuwahi kutoa tafsiri ya alivyolitumia yeye kwenye wimbo wake.. Japo ukiamua kutumia akili za kuunga unga, utaelewa mantiki yake ilikuwa ni kumaanisha 'she got one' - yaani huyo demu amekamilika kwenye kila idara..

Naweza nisiwe sahihi.

Kama alisema hivyo kweli, basi alizingua maana mistari yake hii pekee inamsuta..

"... Kisa, kwa Ngwair ndo amefika
Nami naapa kamwe sintomuacha
Mi nna imani atanizalia mapacha
Na hata kama bahati mbaya akiwa tasa
Mnajua sitoweza kumuacha
Na yote ni sababu tu, she got a gwan.."

Haiwezi kuwa alimaanisha muache aende. Ni tofauti kabisa!
 
Gwan ni neno la kijamaica linalomaanisha 'go on' ila mara nyingi hutumika kwenye sentensi fupi 'wa gwan' kumaanisha 'what is going on'.

Mpaka anafariki dunia, Mangwea hakuwahi kutoa tafsiri ya alivyolitumia yeye kwenye wimbo wake.. Japo ukiamua kutumia akili za kuunga unga, utaelewa mantiki yake ilikuwa ni kumaanisha 'she got one' - yaani huyo demu amekamilika kwenye kila idara..

Naweza nisiwe sahihi.
Unaujua muziki wewe!
 
Sijawahi kuuchoka huu wimbo uko poa beats na kila kitu
Hasa pale anaposema ..."nitomase zake chuchu..."

Ngwea alikuwa mnyama sana katika utunzi, flow, mashairi, na hata kimwonekano aliuishi kimwanamuziki!
 
Back
Top Bottom