Kumbe Shetani Alikuwa Mwandishi wa Habari!, na Alichomfanya Eva Bustani ya Eden ni Uandishi wa Habari?- Je Media Tuombwe Msamaha Kuitwa Shetani au?

Uandishi wa habari ni umbea rasmi uliokubalika kwenye jamii
Mkuu MIXOLOGIST, you are right kazi zozote zinazohusu kusearch for info kuanzia ushushu, investigation, uandishi wa habari na diplomacy, lobbying and advocacy zote kwa namna moja au nyingine zinahusishisha kama umbea fulani ila mtu, familia, jamii na nchi haiwezi kupata maendeleo na ustawi bila kupata taarifa. Information is power.
Tofauti ya habari na umbea, habari ni taarifa constructive na informative za kujenga, wakati umbea ni taarifa destructive za kubomoa kwa vile zote ni taarifa, habari ni taarifa zenye objectivity, impartiality fairness and balance wakati umbea hauna hizo sifa.
P
 
I totally agree, ndiyo maana ni rasmi, yaani unakubalika
 
Umesema dhambi ya asili ni mchakato wa kupata kiumbe kingine; biblia inasema baada ya kuwapulizia pumzi ya uhai akawabariki na kusema "zaeni mkaongezeke". Hebu tuambie process za kuzaa kabla na baada ya hiyo dhambi

Hawezi kukujibu hilo swali. Tatizo la kutoa tafsiri kwa uelewa binafsi ndio linaanziaga hapo. Kajifanya kaelewa zaidi ya kilichoandikwa ktk Biblia ila trust me.. maswali yoyote utakayomuuliza hatoweza kujibu kamwe sana sana ataishia kukutusi tu
 
Kaka Paschal kama kweli ni mkristo mkatoliki basi ni moja ya waumini walei wavivu kusoma na kujifunza imani yao kwa usahihi zaidi. Nasema hivi kwa sababu andiko lako liko kinyume na mafundisho ya kanisa kama tunavyoyafahamu. Vyanzo vya mafundisho rasmi ya kanisa siku hizi viko vingi na viko wazi, nakushauri uweke bidii kutaka kufahamu vyema Imani yako na punguza kuzurura kwenye madhehebu na dini lukuki, unakosa muda wa kutosha na utulivu wa ndani kufanya tafakari na tafakuri za kutosha za Imani yako na habari zake, mambo ya kanisa Katoliki ni mengi, mazito, mazuri na matamu mno, usipokua mtulivu wa kutosha ukatenga na mda wako wa kutosha, ukamshirikisha MUNGU kwa Sala, huwezi kuyaelewa vyema. Mfano, jambo la "dhambi ya asili" kulifahamu vizuri wala huhitaji kuumiza kichwa, katekisimu ya kanisa Katoliki kuanzia fundisho na.396 - 409 limefafanuliwa vyema, huhitaji kutumia kichwa chako kutaka kuhamishia "bahari" kwenye "shimo" la kuchimbwa na kidole kimoja mchangani.
 
Bikira Maria hakuzaa watoto wengine baada ya Kristo. Kwa Mkatoliki kuamini vinginevyo ni kupingana na mafundisho ya Kanisa! Hakuna andiko lolote linalosema Bikira Maria alizaa zaidi ya Yesu na hakuna mapokeo yanayosema hivyo. Paskali kama lipo lililokushawishi kuamini hivyo naomba kufahamu hapa.

Bikira Maria ni bikira daima, Mungu alimtumia kuja duniani, kwa heshima hiyo alimkinga na dhambi ya asili, pia hakuruhusu binadamu mwingine amguse ( refer sanduku la agano ambalo ni kivuli cha Bikira Maria).

Yesu alipokaribia kuitoa roho yake alimuacha mama yake mikononi mwa yule mwanafunzi aliyempenda sana na Maandiko yanasema tangu siku ile alimchukua kwake! How angekuwa amezaa watoto wengine?

Mungu aliingia kwa Bikira Maria na pia alizaliwa na kumuacha Maria akiwa Bikira ( science inagoma lakini kama inavyogoma kuingia kwa mimba bila kujamiiana basi na hili wajue aliyefanya ni Mungu asiyeshindwa).

Pascal Mayalla usingekuwa Mkatoliki nisingeomba ufute hiyo sentensi lakini kwa nafasi yako na ukitumia jina lako halisi umesigina moja ya fundisho muhimu la Kanisa! Uungu wa Yesu kulikopingwa karne nyingi ndicho chanzo cha kupingwa kwa mafundisho mengi juu ya Bikira Maria maana ndiyo sehemu ya kudhibitisha safari yetu ya wokovu iliyohitimishwa kwa kuteswa, kufa na kufufuka kwa Kristo.
 
una mapepo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].. yani nyie machoko akili zenu zipo kwenye kulaghai watu na hizo mambo sasa kama ninamapepo kwanini usiende kwa mwamposa aniombee nikatoe ushuhuda pale mbele mnapotoaga sadaka kwa mafungu..

"Eti wenye elfu 50 pita mbele nina makmbi yenu.. wanaofata wenye elfu 40.. then 30k 10k mtakuwa wa mwisho.. alafu hakikisheni wote mmenunua mafuta na maji ya baraka.."

Hakuna kitu naweza sema nakosea hapa hata mkisema ni mapepo ya uandishi wa habari pia..[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kilichofanyika kwenye bustani ya Eden siyo uandishi wa habari bali yalifanyika matusi... (Walikualana)
 
Kwa mara ya kwanza nimekuona kuwa u mweupe sana kwa mambo ya Imani....umeandika kwa kirefu sana Kaka yangu Paskali lakini umepotosha maandiko!!

Na Mungu anasema ole wake yeye atakayeongeza maneno haya.


Kwanza usimpe shetani ukubwa kuwa anaweza kujigeuza kuwa kuimbe fulani, hapana ana uwezo wa kuingia tu, au kumtumia kiumbe fulani, pili shetani kamwe hawezi kujigeuza kuwa Mungu no way....ni wachanga wa imani tu wanasimtambua shetani akijifanya malaika mwema.

Tangu mwanzo, na Yesu alisisitiza Mungu alimwumba mtu mke na mtu mume akawafanya kuwa mwili mmoja akawaruhusu kuzaliana, please go and read the Bible onve more.

Hivi katika akili yako ya kawaida unafikiri Mungi aliumba watu wapea tofauti ili iweje? Mungu akaumba wanyama wa pea tofauti ili iweje?


Yaani amewaumba watazamane tu na wasaidiane tu sijui kwa lipi? Kuituza bustani?

Dhambi ya asili ni kukosa utii,. Mungu alikataza kula tunda la mti wa katikati period, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na hakukuwa na nguo, walipokula tunda wakajiona kuwa wako uchi.

Nitarudi.

Nimejikuta nimechukiaaa, hata wewe, unayejiita mkristo unaongea vitu vya tofauti na maandishi.
 

Kuna makosa mengi ya kutisha biblia imeandika, ikiwemo dhambi ya Daudiya uzinzi wa mke wa mtu na mauaji, ubakaji wa kabila la Benjamin kule Gibea.

Hata neno uchi linatajwa bila staha.
 
Mwandishi wa habari anaetakiwa atumie njia mbalimbali ili apate habari. Anatakiwa awe kama kinyonga. Shetani alitumia mbinu ili kumshawishi Eva. Kwa mantiki hiyo shetani alikuwa amefuzu katika mambo ya habari. Sioni kosa la mchungaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna makosa mengi ya kutisha biblia imeandika, ikiwemo dhambi ya Daudiya uzinzi wa mke wa mtu na mauaji, ubakaji wa kabila la Benjamin kule Gibea.

Hata neno uchi linatajwa bila staha.
Ni Kweli,
Namshangaa huyu ndugu anaepotosha kuwa biblia ilificha
 
🙌🙌🙌
 
Duuuh! Kwahiyo u katoliki hautambui kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake??
Biblia inatuambia kwamba Yesu alikuwa na ndugu wanne: Yakobo, Yusufu, Simioni na Yuda ( Mathayo 13:55-56)55. Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
56. Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?

Yusufu hakulala na MARIAMU alipokuwa na ujauzito wa Yesu,( Mathayo 1:25)baada ya Hapo ndoa yake iliendelea kama kawaida!! Haikuwa na sababu ya Kuendelea Kubaki kwa Yusufu kama Aliendelea kuwa bikra. Tufungue Ufahamu hata kidogo tulitafakari hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…