Kumbe Shetani Alikuwa Mwandishi wa Habari!, na Alichomfanya Eva Bustani ya Eden ni Uandishi wa Habari?- Je Media Tuombwe Msamaha Kuitwa Shetani au?

Kumbe Shetani Alikuwa Mwandishi wa Habari!, na Alichomfanya Eva Bustani ya Eden ni Uandishi wa Habari?- Je Media Tuombwe Msamaha Kuitwa Shetani au?

Uandishi wa habari ni umbea rasmi uliokubalika kwenye jamii
Mkuu MIXOLOGIST, you are right kazi zozote zinazohusu kusearch for info kuanzia ushushu, investigation, uandishi wa habari na diplomacy, lobbying and advocacy zote kwa namna moja au nyingine zinahusishisha kama umbea fulani ila mtu, familia, jamii na nchi haiwezi kupata maendeleo na ustawi bila kupata taarifa. Information is power.
Tofauti ya habari na umbea, habari ni taarifa constructive na informative za kujenga, wakati umbea ni taarifa destructive za kubomoa kwa vile zote ni taarifa, habari ni taarifa zenye objectivity, impartiality fairness and balance wakati umbea hauna hizo sifa.
P
 
I totally agree, ndiyo maana ni rasmi, yaani unakubalika
 
Umesema dhambi ya asili ni mchakato wa kupata kiumbe kingine; biblia inasema baada ya kuwapulizia pumzi ya uhai akawabariki na kusema "zaeni mkaongezeke". Hebu tuambie process za kuzaa kabla na baada ya hiyo dhambi

Hawezi kukujibu hilo swali. Tatizo la kutoa tafsiri kwa uelewa binafsi ndio linaanziaga hapo. Kajifanya kaelewa zaidi ya kilichoandikwa ktk Biblia ila trust me.. maswali yoyote utakayomuuliza hatoweza kujibu kamwe sana sana ataishia kukutusi tu
 
Wanabodi

Declaration of Interest
Mimi ni Mkristu Mkatoliki, ila mara moja moja huwa nahudhuria mafundisho katika madhehebu mbalimbali, ikiwemo Lutheran, Anglican, Makanisa ya Wokovu, na kwa wachungaji mbalimbali akiwemo Nabii Mwingira, Askofu Kakobe, Mzee wa Upako, Mwamposa, Assemblies of God, na hadi mihadhara ya Kiislamu.

Angalizo za Kiimani Kwa Open Minded na Closed Minded.
Kwenye mambo ya imani, kuna watu wa aina mbili, open minded na closed minded.
Open minded ni wale waumini wanaoamini dini with an open mind, hata akitokea mtu wa imani nyingine kinyume na imani yako, you can listen and try make sense out of it. Hili ndio bandiko Lao.

Lakini kuna closed up people ambao wakiaminishwa dini yao, wao wanaamini ni Mungu mwenyewe, hivyo hata ukiwaambia vitabu vya dini vimeandikwa na binadamu na kuhaririwa, hawawezi kuamini wanaamini ni Mungu ndio kuaandika hivyo ukileta jambo lolote ambalo wao hawalijui, watakuona kama ni una kufuru, watu hawa closed minded naombeni muishie hapa maana huko mbele mtaishia kuumia kiimani, just keep on believing what you believe.

Biblia ni kitabu kitakatifu cha dini ya Kikristu, wakati yaliyoandikwa kwenye Bibilia yanatendeka, kuna mengine ni mambo mabaya kabisa hayaandikiki, bila staha hivyo kwenye Bibilia kuna baadhi ya mambo yameandikwa lugha ya picha na tamathali za semi kwa la kuweka staha, moja ya mambo hayo ambayo yameandikwa Kwa staha ni ile dhambi ya asili, the original sin, kumaanisha sisi binadamu asili yetu ni dhambi fulani lazima itendeke ndipo kiumbe kizaliwe. Kwa sisi Wakristu Wakatoliki, dhambi hiyo ya asili huondolewa kwa sacrament ya Ubatizo na mapadri, masista, makasisi wetu na maaskofu wetu hawaruhusiwi kuitenda!.

Moja ya jambo lililoandikwa Kwa staha kubwa kwenye Bibilia ni kuhusu dhambi ya asili, "the original sin" ya Mama yetu Eva kushawishiwa na shetani, ale lile tunda walilokatazwa na Mungu wasilile.

Shetani akajigeuza nyoka, akapenya Bustanini, kuna kitu hakikusemwa kwenye Bible, lakini kupitia the powers of information powers, sisi baadhi yenu tumejaaliwa kuwa nazo, hivyo tunauwezo wa kuvijua baadhi ya vitu ambavyo vilitokea lakini haviku jandikwa ili kutunza staha!.

Shetani baada ya kujigeuza nyoka na kupenya Bustanini, si wengi wanafahamu kuwa shetani ni bingwa wa kuji disguise, na anaweza kuji disguise kuwa kiumbe chochote na hata kuji disguise as God na akaponya watu na kufanya miujiza!, na kuna mara kibao shetani ana ji disguise as God, na kufanya ishara na miujiza ili watu wamwamini na kumfuata na kumwabudu, hivyo kuna wengi wanamwabudu shetani disguised as God bila wao kujijua, wakidhani wanamwabudu Mungu wa Kweli!.

Hivyo shetani baada ya kujigeuza nyoka na kufanikiwa kupenya Bustanini, kabla hajamtokea Eva, alijigeuza, kiumbe kingine, ndipo akamtokea Eva! na Eva akashituka sana kuona kuna mtu mwingine zaidi ya Adam!, na hapo ndipo ushawishi ukaanza na katika kumshawishi Eva kula lile tunda, shetani alimshawishi sio kwa maneno tuu bali na kwa matendo practically ikiwemo kulichuma hilo tunda akalishika na kumuonyesha Eva jinsi tunda linavyomegwa na akamegea Eva na shetani na wakala kwanza tunda wao Eva na shetani na baada ya Eva kuonja utamu wa lile tunda, ndio sasa akaenda Kwa Adamu kumpelekea tunda na kumshawishi Adam kwa kumuonyesha jinsi tunda linavyomegwa na kumlazimisha Adamu kumega practically nae Adamu akamega tunda kisha, wakaishia zao usingizini, walipoamshwa ndipo wakajishtukia kuwa wako uchi baada ya kujua kazi ya vile viungo vya ule mti wa katikati na kumega tunda, na hapo ndipo ikawa wametenda dhambi ya asili, yaani the original sin!. Na adhabu yako sasa ni kufukuzwa Bustanini na Mwanamke atazaa kwa uchungu kufidia kumshawishi Adamu kumega tunda, hivyo wale wanawake wanaozaa kwa ceaserian by preference ili kukwepa maumivu ni wanatenda dhambi bila kujitambua.

Hivyo dhambi ya asili sio sio mti sio tunda, sio neno "mega tunda" au "kula tunda la mti wa katikati" ni "tendo" la kukatazwa usifanye jambo fulani, wewe ukalifanya hivyo dhambi ya asili ni tendo la tunda kumegwa na kuliwa.

Bible haikusema dhambi ya asili ni tendo, expressly kwa uwazi kwa lengo la staha, ila bible imesema kuhusu dhambi ya asili ni tendo kwa impliedly kuwa kuna tendo fulani lazima litendwe ili mwanamke spate ujauzito ili binadamu mpya azaliwe, tendo hilo ndio dhambi ya asili, ni lazima hiyo dhambi ya asili itendwe na mwanamume na Mwanamke ndipo kiumbe kipya kiumbike!.

Shetani katika kumrubuni Eva, akamwambia wakila tunda, watakuwa na uwezo wa Kimungu wa kuumba viumbe wengine!.

Kuna binadamu mmoja tuu, Bikira Maria, yeye ndiye pekee aliye kingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huku akiwa bado ni bikira bila ile dhambi ya asili kutendwa ya kumegwa kwa tunda, hivyo mtoto Yesu alizaliwa bila dhambi ya asili kutendwa!, na Bikira Maria alisikia dalili ya uchungu lakini alimzaa Yesu bila uchungu, ila baada ya kumzaa Yesu, ndoa yake iliendelea kikawaida na akapata watoto wengine kwa njia ya kawaida.

Kitendo cha kiongozi mmoja wa dini ya wokovu mwenye wafuasi wengi hapa jijini DAR kusema kilichofanyika kule bustani ya Eden ni Uandishi wa habari na kuwa Shetani ni Mwandishi wa habari, hakiwezi kuachwa kipite hivi hivi bila kupingwa.

Kwa sasa tuko katika ulimwengu kimtandao, cyber world ambapo kila mwenye access na mtandao, anakuwa ni mtoa habari na msambaza habari, kwa kuweza kupost chochote kwenye mitandao na kikawafikia watu wengi kwa haraka lakini sio wote ni waandishi wa habari. bali sasa kila mtu ni mpashanaji wa habari!.

Kitendo alichokifanya Mtumishi wa Mungu, Boniface Mwamposa kutangaza kuwa shetani alikuwa ni Mwandishi wa habari, sio kututendea haki sisi waandishi wa habari na tasnia nzima ya habari.
Kwa hisani ya mwana jf JanguKamaJangu Mtumishi Boniface Mwamposa asema "Shetani alikuwa Mwandishi wa habari"

Kitendo hiki cha kusema shetani alikuwa Mwandishi wa habari na kilichofanyika kwenye bustani ya Eden kwenye ile dhambi ya asili ni uandishi wa habari, sio kututendea haki sisi waandishi wa habari na tasnia yetu nzima ya habari. Shetani hakuwa Mwandishi wa habari, wala kitendo kile cha kumrubuni Eva sio uandishi wa habari ni ulaghai tuu katika upashanaji wa habari.

Kufuatia mabaliko ya dunia kuwa ni dunia mtaandao, cyber world sasa kila mtu anaweza kuandika chochote na kusambaza chochote au habari zozote kwenye mitandao na kuonekana kama Mwandishi wa habari, lakini sii Mwandishi wa habari.

Lengo la Mtumishi Mwamposa ni zuri kuhusu umuhimu wa sisi waandishi wa habari ni watu muhimu sana, Ila pia ni watu hatari Sana, pale kalamu zetu zikitumika vibaya zinaweza kuleta majanga makubwa, lakini shetani hakuwa Mwandishi wa habari na kilichofanyika kwenye bustani ya Eden sio uandishi wa habari!.

Kufuatia powers alizonazo Mwamposa, kitendo cha kumuita shetani ni Mwandishi wa habari, kinaweza kikapelekea sisi waandishi wa habari tukaanza kuitwa mashetani!, jee sisi waandishi wa habari, na tasnia nzima ya habari, tunakubali kuitwa mashetani, na tukanyamaza tuu au to demand an apology kutoka kwa Mwamposa kutuomba radhi waandishi kwa kumsingizia shetani kuwa alikuwa ni Mwandishi wa habari, na chanzo cha dhambi ile ya asili pale Bustanini Eden ni Mwandishi wa habari shetani?.

Paskali
Kaka Paschal kama kweli ni mkristo mkatoliki basi ni moja ya waumini walei wavivu kusoma na kujifunza imani yao kwa usahihi zaidi. Nasema hivi kwa sababu andiko lako liko kinyume na mafundisho ya kanisa kama tunavyoyafahamu. Vyanzo vya mafundisho rasmi ya kanisa siku hizi viko vingi na viko wazi, nakushauri uweke bidii kutaka kufahamu vyema Imani yako na punguza kuzurura kwenye madhehebu na dini lukuki, unakosa muda wa kutosha na utulivu wa ndani kufanya tafakari na tafakuri za kutosha za Imani yako na habari zake, mambo ya kanisa Katoliki ni mengi, mazito, mazuri na matamu mno, usipokua mtulivu wa kutosha ukatenga na mda wako wa kutosha, ukamshirikisha MUNGU kwa Sala, huwezi kuyaelewa vyema. Mfano, jambo la "dhambi ya asili" kulifahamu vizuri wala huhitaji kuumiza kichwa, katekisimu ya kanisa Katoliki kuanzia fundisho na.396 - 409 limefafanuliwa vyema, huhitaji kutumia kichwa chako kutaka kuhamishia "bahari" kwenye "shimo" la kuchimbwa na kidole kimoja mchangani.
 
Bikira Maria hakuzaa watoto wengine baada ya Kristo. Kwa Mkatoliki kuamini vinginevyo ni kupingana na mafundisho ya Kanisa! Hakuna andiko lolote linalosema Bikira Maria alizaa zaidi ya Yesu na hakuna mapokeo yanayosema hivyo. Paskali kama lipo lililokushawishi kuamini hivyo naomba kufahamu hapa.

Bikira Maria ni bikira daima, Mungu alimtumia kuja duniani, kwa heshima hiyo alimkinga na dhambi ya asili, pia hakuruhusu binadamu mwingine amguse ( refer sanduku la agano ambalo ni kivuli cha Bikira Maria).

Yesu alipokaribia kuitoa roho yake alimuacha mama yake mikononi mwa yule mwanafunzi aliyempenda sana na Maandiko yanasema tangu siku ile alimchukua kwake! How angekuwa amezaa watoto wengine?

Mungu aliingia kwa Bikira Maria na pia alizaliwa na kumuacha Maria akiwa Bikira ( science inagoma lakini kama inavyogoma kuingia kwa mimba bila kujamiiana basi na hili wajue aliyefanya ni Mungu asiyeshindwa).

Pascal Mayalla usingekuwa Mkatoliki nisingeomba ufute hiyo sentensi lakini kwa nafasi yako na ukitumia jina lako halisi umesigina moja ya fundisho muhimu la Kanisa! Uungu wa Yesu kulikopingwa karne nyingi ndicho chanzo cha kupingwa kwa mafundisho mengi juu ya Bikira Maria maana ndiyo sehemu ya kudhibitisha safari yetu ya wokovu iliyohitimishwa kwa kuteswa, kufa na kufufuka kwa Kristo.
 
una mapepo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].. yani nyie machoko akili zenu zipo kwenye kulaghai watu na hizo mambo sasa kama ninamapepo kwanini usiende kwa mwamposa aniombee nikatoe ushuhuda pale mbele mnapotoaga sadaka kwa mafungu..

"Eti wenye elfu 50 pita mbele nina makmbi yenu.. wanaofata wenye elfu 40.. then 30k 10k mtakuwa wa mwisho.. alafu hakikisheni wote mmenunua mafuta na maji ya baraka.."

Hakuna kitu naweza sema nakosea hapa hata mkisema ni mapepo ya uandishi wa habari pia..[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kilichofanyika kwenye bustani ya Eden siyo uandishi wa habari bali yalifanyika matusi... (Walikualana)
 
Kwa mara ya kwanza nimekuona kuwa u mweupe sana kwa mambo ya Imani....umeandika kwa kirefu sana Kaka yangu Paskali lakini umepotosha maandiko!!

Na Mungu anasema ole wake yeye atakayeongeza maneno haya.

Kwanza usimpe shetani ukubwa kuwa anaweza kujigeuza kuwa kuimbe fulani, hapana ana uwezo wa kuingia tu, au kumtumia kiumbe fulani, pili shetani kamwe hawezi kujigeuza kuwa Mungu no way....ni wachanga wa imani tu wanasimtambua shetani akijifanya malaika mwema.

Tangu mwanzo, na Yesu alisisitiza Mungu alimwumba mtu mke na mtu mume akawafanya kuwa mwili mmoja akawaruhusu kuzaliana, please go and read the Bible onve more.

Hivi katika akili yako ya kawaida unafikiri Mungi aliumba watu wapea tofauti ili iweje? Mungu akaumba wanyama wa pea tofauti ili iweje?

Yaani amewaumba watazamane tu na wasaidiane tu sijui kwa lipi? Kuituza bustani?

Dhambi ya asili ni kukosa utii,. Mungu alikataza kula tunda la mti wa katikati period, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na hakukuwa na nguo, walipokula tunda wakajiona kuwa wako uchi.

Nitarudi.

Nimejikuta nimechukiaaa, hata wewe, unayejiita mkristo unaongea vitu vya tofauti na maandishi.
 
Ua

Uandikwaji wa kistaha katika biblia huandwikwa kwa namna ya kutokupoteza maana halisi ya Jambo.:- Eg Genesis 4:1.
NLT
Now Adam had sexual relations with his wife, Eve, and she became pregnant. When she gave birth to Cain, she said, “With the Lord’s help, I have produced a man!”

Kuna makosa mengi ya kutisha biblia imeandika, ikiwemo dhambi ya Daudiya uzinzi wa mke wa mtu na mauaji, ubakaji wa kabila la Benjamin kule Gibea.

Hata neno uchi linatajwa bila staha.
 
Mwandishi wa habari anaetakiwa atumie njia mbalimbali ili apate habari. Anatakiwa awe kama kinyonga. Shetani alitumia mbinu ili kumshawishi Eva. Kwa mantiki hiyo shetani alikuwa amefuzu katika mambo ya habari. Sioni kosa la mchungaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna makosa mengi ya kutisha biblia imeandika, ikiwemo dhambi ya Daudiya uzinzi wa mke wa mtu na mauaji, ubakaji wa kabila la Benjamin kule Gibea.

Hata neno uchi linatajwa bila staha.
Ni Kweli,
Namshangaa huyu ndugu anaepotosha kuwa biblia ilificha
 
Kwa mara ya kwanza nimekuona kuwa u mweupe sana kwa mambo ya Imani....umeandika kwa kirefu sana Kaka yangu Paskali lakini umepotosha maandiko!!

Na Mungu anasema ole wake yeye atakayeongeza maneno haya.

Kwanza usimpe shetani ukubwa kuwa anaweza kujigeuza kuwa kuimbe fulani, hapana ana uwezo wa kuingia tu, au kumtumia kiumbe fulani, pili shetani kamwe hawezi kujigeuza kuwa Mungu no way....ni wachanga wa imani tu wanasimtambua shetani akijifanya malaika mwema.

Tangu mwanzo, na Yesu alisisitiza Mungu alimwumba mtu mke na mtu mume akawafanya kuwa mwili mmoja akawaruhusu kuzaliana, please go and read the Bible onve more.

Hivi katika akili yako ya kawaida unafikiri Mungi aliumba watu wapea tofauti ili iweje? Mungu akaumba wanyama wa pea tofauti ili iweje?

Yaani amewaumba watazamane tu na wasaidiane tu sijui kwa lipi? Kuituza bustani?

Dhambi ya asili ni kukosa utii,. Mungu alikataza kula tunda la mti wa katikati period, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na hakukuwa na nguo, walipokula tunda wakajiona kuwa wako uchi.

Nitarudi.

Nimejikuta nimechukiaaa, hata wewe, unayejiita mkristo unaongea vitu vya tofauti na maandishi.
🙌🙌🙌
 
Bikira Maria hakuzaa watoto wengine baada ya Kristo. Kwa Mkatoliki kuamini vinginevyo ni kupingana na mafundisho ya Kanisa! Hakuna andiko lolote linalosema Bikira Maria alizaa zaidi ya Yesu na hakuna mapokeo yanayosema hivyo. Paskali kama lipo lililokushawishi kuamini hivyo naomba kufahamu hapa.

Bikira Maria ni bikira daima, Mungu alimtumia kuja duniani, kwa heshima hiyo alimkinga na dhambi ya asili, pia hakuruhusu binadamu mwingine amguse ( refer sanduku la agano ambalo ni kivuli cha Bikira Maria).

Yesu alipokaribia kuitoa roho yake alimuacha mama yake mikononi mwa yule mwanafunzi aliyempenda sana na Maandiko yanasema tangu siku ile alimchukua kwake! How angekuwa amezaa watoto wengine?

Mungu aliingia kwa Bikira Maria na pia alizaliwa na kumuacha Maria akiwa Bikira ( science inagoma lakini kama inavyogoma kuingia kwa mimba bila kujamiiana basi na hili wajue aliyefanya ni Mungu asiyeshindwa).

Pascal Mayalla usingekuwa Mkatoliki nisingeomba ufute hiyo sentensi lakini kwa nafasi yako na ukitumia jina lako halisi umesigina moja ya fundisho muhimu la Kanisa! Uungu wa Yesu kulikopingwa karne nyingi ndicho chanzo cha kupingwa kwa mafundisho mengi juu ya Bikira Maria maana ndiyo sehemu ya kudhibitisha safari yetu ya wokovu iliyohitimishwa kwa kuteswa, kufa na kufufuka kwa Kristo.
Duuuh! Kwahiyo u katoliki hautambui kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake??
Biblia inatuambia kwamba Yesu alikuwa na ndugu wanne: Yakobo, Yusufu, Simioni na Yuda ( Mathayo 13:55-56)55. Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
56. Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?

Yusufu hakulala na MARIAMU alipokuwa na ujauzito wa Yesu,( Mathayo 1:25)baada ya Hapo ndoa yake iliendelea kama kawaida!! Haikuwa na sababu ya Kuendelea Kubaki kwa Yusufu kama Aliendelea kuwa bikra. Tufungue Ufahamu hata kidogo tulitafakari hili
 
Back
Top Bottom