Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...

Yaani pasco uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo? Too bad!
 
Kama siku umeleta utumbo kwenye baraza hili basi hii ndio utumbo uliopita yote. Kwa yoyote aliezaliwa Zanzibar, na sio memba wa maskani ya Kisonge au "wakuja" atakwambia video yako ni ya kupika na mpishi tunamjua.

Sote tunajua nani kamuua Karume na kwa sababu gani.Mauaji ya Karume yalikuwa hayana malengo ya kubadilisha utawala yalikuwa na malengo ya kumuondoa mtawala. Ukuiljua hilo inatosha ya kujibu utumbo wako hapo juu.Vilevile unajua watu kadhaa waliotuhumiwa kushiriki mauaji walipewa " hifadhi bara" na hata hapo Alhaj Jumbe alipojitahidi kuwaomba washtakiwa kwena Zanzinzibar kujibu mashtaka walikingiwa kifua na bara. Mtuhumiwa mkubwa kuliko wote alikuwa Col. Ali Mahfoudh, ambae alikuwamtu wa kwanza kufika sehemu ya aliouwa Mzee Karume, na kuupiga teke maiti ya muuaji, Humud na kusema " bloodyful". Baadae Col. Mahfoudh alipandishwa cheo! Tunajua ni kwa nini matokeo ya uchaguzi yanakuwa kama yanavyokuwa. Hayana mkono wa Jamshid wala Oman yana mkono wa Tanganyika kuendelea kuitawala Zanzibar na kuzimeza rasilimali zake.

Sipingi kama Jamshid alifurahi alipouliwa Karume, lakini watu hao walikuwa wengi, fanya utafiti zaidi na hasa Tanganyika. Kuna kiongozi mmoja wa Tanganyika hakuweza kuzizia hisia zake na kusema " jinamizi " limeondoka. Kuna watu wamepika pilau Zanzibar na wengine kunyongeka na hili ni jambo la kawaida kwa msiba wowote ambapo utokeaji wake unaweza kuleta faraja au kutokea kwake kutaleta majonzi u furaha.

Msiwafanye wazanzibari mazuzu kiasi hicho. Mbinu hizi zinajirejea tu kupumbaza ili kumficha adui wa kweli wa Zanzibar. Nakuheshimu lakini kwa video ya kuungwa ungwa na kuwekwa vionjo kwenye midomo ya watu hayo sio tu hayanogi lakini umeonesha rangi zako halisi. Sikuamini tena
 
kuhusu seif kushinda siku zote hlo halina shaka,tatizo 'hatuwapi' kwa aina ya 'utu' walio nao
 
Mkuu you are misled!
Maalim is a goner!
Maalim amekuwepo si leo, bali jana na juzi na kila mara amekuwa akifungwa goli la uhakika bila matatizo.
Maalim ni mteja wa CCM!
As for arms, jiridhishe na kifua kilchokuwepo visiwani wakati wa uchaguzi!!!
 
Ntarudi baadae,huyu sultan nilimsoma juu juu tu,hata hivyo ataendelea kuziwekea kivuli siasa za Zanzibar mpaka pale wahafidhina uchwara wa Ccm watakapotangulia mbele ya haki,vijana wengi hawana habari na propaganda za ccm
 
Pasco,
Jamshid
kufurahia kifo cha Karume si jambo la kupendeza na si kitu cha
sisi leo kukipa uzito.

Ila nashindwa kufanya mjadala wowote wa maana kwa kuwa katika maandishi
yako hakuna ''sense,'' ila ni ushabiki.

Tabu sana kujadili ushabiki.
Nimekuja hapa kwa moja tu nalo ni kuhusu Usultani Zanzibar.

Nimezungumza na wanasiasa wa juu kabisa katika Zanzibar na watu waliopigania
uhuru wa Zanzibar na wote walinambia kuwa kuondolewa kwa Sultani Zanzibar
lilikuwa jambo la muda tu.

Wanasema Sultani asingeweza kuwa na maana yoyote katika siasa zile za 1960.
 
Juzi waarabu saba wameuana mwanza

juzi waarabu wamembaka binti guest


Siku kadhaa waarabu wafugaji wameuana na waarabu wakulima


Muarabu mwenye macho mekundu anauliwa waarabu wenzake eti mchawi

Muarabu albino anauwawa eti ni dili kwa waarabu weusi
 

Hizo ni sababu za ccm kujihalalishia kutawala. Kweli mtu mzima na akili anaamini kama waarabu wanataka kurudi zanzibar zama hizi! Mbona wanaofurahia vifo vya wenzao ni wengi tu, hata ccm wanafurahia kuuwa wapinzani na ndio maana huimarisha jeshi wakati wa uchaguzi! ikiwa serikali iko tayari kuuwa raia wake kuna nini cha kushangaza kwa mtu kufurahia kifo cha wa mbali. CCM watafute njia nyengine za kudanganya watu wa zama hizi, mbinu hizi zilitumika nyima ila sasa kila mtu anaelewa ukweli, si wakati wa kuburuzwa tena.
 
Karibu na endelea kwa kasi hiyo hiyo na ari, usichoke
 
Nimezungumza na wanasiasa wa juu kabisa katika Zanzibar na watu waliopigania
uhuru wa Zanzibar na wote walinambia kuwa kuondolewa kwa Sultani Zanzibar
lilikuwa jambo la muda tu.
Nafikiri umezungumza na wana mapinduzi wa Maskani ya Kisonge! Sultan Zanzibar kaondoka hakupinduliwa. Aliepundiliwa ni serikali ya Moh' d Shamte. Jamshid kaondoka Zanzibar saa sita akiisubiri meli ya MV. Salama kutoka Dsm ikifanya safari za kawaida,ilifika na kutia nanga , ikashusha abiria na watu wakaelezwa yaliotokea. Wengine walishuka na wengine hawakushuka wakaondoka na Jamshid. Wakati huo Mhammed Shamte na baraza la mawaziri wote wameshakamatwa. Kama lengo ni Jamshid kwa nini hawakumkamata?
 
ccm wanatapatapa kutafuta kuungwa mkono na kupunguza hasira za watu ila wamechelewa.Wamechukua madaraka kwa nguvu lkn bado wanaumia wakiona support na mapenzi ya wazanzibar kwa maalim!
 
Hahahahaah!! Pasco wakati mwingine nabaki nacheka tu.

Wewe umezaliwa Magu wakati huo ilikuwa Wilaya ya Mwanza, Pwani umekuja baada ya Mzee kuja kufanya kazi kwa waungwana cha kuchekesha unawafundisha watu wa pwani historia ya mapinduzi ya Zanzibar daah!

Ni sawa mtu atoke Kengeja Zanzibar, mpaka Misungwi Mwanza, awafundishe wasukuma historia ya Mwanamarundi.
 
Mapinduzi matukufu Zanzibar yanaendelea tu kuanzia 1964........ 2000, 2005,2010,2015 - kitu kimoja kinayaendesha haya mapinduzi - kupindua maamuzi ya sanduku la kura
 
Thread za kipumbavu.kwann mnataka kutugawa? Wote tunapita hapa duniani waasisi wapo wapi?njaa zisitutoe utu.unamuwaza sultani tu mbona humuwazi mjerumani
 
Haya ulioyasema humu ndio yale nilioyasema humu kuwa
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa!, walijiondokea wenyewe!, hakuna yoyote aliyekuwa akimtafuta sultani ni uoga tuu ndio ulimkimbiza!.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…