Baba ni baba
Senior Member
- Dec 19, 2014
- 113
- 50
Mnyama kula vyako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna siku nilimuona kwenye private car anavuta sigara nilimuonea huruma sana!naona rachel anapita kila njia na hatua alizopita role model wake ray -c safi .......
huyu si alitangazaga anaona mwaka jana? ile ndoa sijui iliyeyukia wapi.....
Wasanii wa zamani wanarudi kivingine
GK-diva
T.I.D- recho
Bushoke- jini kabula
Kuna siku nilimuona kwenye private car anavuta sigara nilimuonea huruma sana!
Juma nature - lady jaydee
Chege- flora mbasha
wote ni waathirika wa ile kitu mbayaMALOVEE? Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed TID au Mzee Mnyama na mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat Recho THT, wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni wa kimapenzi, Ijumaa Wikienda limeinusa. Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali huku wakidaiwa kupiga mitungi kiasi cha kushindwa kuzificha hisia zao.Mbona ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena wanapopiga mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja mjini Dodoma, waliponda raha kinomanoma, kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana mashosti zake wa karibu. Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani, halafu pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata mambo meupe anatumia, alisema shosti huyo. Baada ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini kwake THT, Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana muda mrefu hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi. Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu wangu kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila ninapokuwa na mwanaume wanasema ni bwanangu kitu ambacho si cha kweli kama wanavyonizushia kuvuta bangi. THT siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe. Nimekuja kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia uongo, alisema Recho. Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo. Dah...! Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye, alisema TID.