Wimbo
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 866
- 625
Kumbe Watanzania tuna woga na siyo amani, hoja ndogo tu tena ya nia njema ya kutukwamua mahali tulipo DP world tunatukanana mpaka mapovu yanatutoka.
Hivi katika Dunia hii walioweza kufanikiwa bila kusubutu ni Taifa lipi kwa mfano. kelele ngapi zilizopigwa Chuma aliposema tunahamia Dodoma?
Kelele ngapi zilipigwa aliposema tunajenga bwawa la Nyerere anayetaka asitake tunajenga , maendeleo makubwa tunayoyaona Duniani hata madege na mameli ya kutisha baharini yalianza kwa kusubutu.
Nani aliota ndoto za kigongo Busisi kutandikwa daraja, lazima kusubutu na alichotujengea Chuma ni uthubutu, mimi sina kauli za umaskini tena sisi ni matajiri. umaskini wetu uko vichwani.
Mama twende zetu mbele kwa mbele Kikwete alisema,"huwezi kula bila kuliwa" tutaliwa kidogo lakini na sisi tutakula, DRC CONGO wanatusubili tufanye maamuzi sahihi Burundi, Malawi Uganda hata Kenya.
Tupunguze malumbano tuchape kazi.
Mama kwani hawa Dp wanaanza lini?