Kumbe tozo zililetwa ili kushindana mapato wanayopata mitandao ya simu na mabenki?

Kumbe tozo zililetwa ili kushindana mapato wanayopata mitandao ya simu na mabenki?

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Hebu tuzitafakari hizi kauli mfu za Naibu Spika:
"Wananchi wengi wanalalamikia kodi iliyowekwa na Serikali, hawatizami mapato yanayokatwa na benki, hawatizami mapato yanayokatwa na kampuni za simu. Lazima iwe regulated [idhibitiwe].”
"Benki unatuma pesa wanachukua pesa nyingi zaidi ya Serikali kwa asilimia kubwa sana, lakini Serikali inayojenga madarasa ndiyo inalaumiwa. Kwa hiyo kuna kizingiti ambacho kinatengenezwa kuipiga dongo Serikali wakati pesa wanachukua watu wengine."
"Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema Serikali inayojenga madarasa inalaumiwa kuhusu tozo kuliko kampuni za simu na benki ambazo zinakata makato makubwa zaidi."
Ukizifikiria hizi kauli za Naibu Spika, utagundua ni kama serikali inaona gere kwa mapato wanayopata makampuni ya simu na mabenki kwenye miamala tunayoifanya wananchi.

Na ndiyo maana mara ya kwanza kabisa tozo zilipoletwa mwaka jana zilikuwa zinakaribiana sana na makato yale halali. Ukijumlisha na VAT wanayopata serikali basi ilikuwa ni kama tozo zinaendana sawasawa na makato ya muamala husika.

Hii thinking ya dunia ya ngapi? Kwamba kwa kuwa makampuni yanapata kikubwa kutoka kwa wananchi, basi ngoja tukapige mulemule na sisi tujipatie sawa sawa na wao bila kujali wanazidi kumkamua mwananchi?

Sasa kwa taarifa yake, siyo kwenye haya makato ya kidigitali tu, bali karibu sekta zote private entities ndizo zinapiga faida kubwa kuwazidi public entities. Na hiyo yote inasababishwa na wao wanasiasa, wanakuwa wanaingilia maamuzi ya professionals mwisho wa siku hao wataalamu wanaanza kufanya kazi kwa kuangalia upepo wa siasa unaelekea wapi na sio kitaalamu tena.

Wataalamu wetu wengi maofisini wamelishwa sumu ya u-ccm, yani maamuzi wanayofanya wanaangalia kwanza upepo wa siasa umekaaje. Nakumbuka sehemu moja nilihudhuria wakati wafanyakazi wapya wanafanyiwa induction, nilishangaa sana kumkuta mkurugenzi amekaa na ilani ya ccm mezani wakati huohuo hana kijaribu cha mission na visions za taasisi yake.

Mfano mdogo tuu, kwenye sekta ya afya hospitali binafsi ndizo zinapata pesa ndefu zaidi kutoka NHIF kushinda hospitali za umma. Mpaka juzi juzi NHIF wamelalamika kwamba eti kuna ujanja ujanja hawa private hospitals wanafanya, lakini ukweli ni kwamba hakuna ujanja wowote bali tuu inawauma privates kupata pesa nyingi kuzishinda public hospitals.

Sasa kwa akili kama hizi za wanasiasa wetu, tusitegemee kupiga hatua yoyote.

Serikali haiangalii uwekezaji iliofanya taasisi za kifedha au taasisi yoyote ile ndo maana unaona kodi zimekaa kikandamizi sana...kodi zipo juu sana...huwezi kukuza mtaji Tanzania kama haukwepi kodi...
 
Ule mradi uliokuwa unaitwa "Mkonga wa Taifa" tuliambiwa Data zutashuka bei au ni Sound za CCM kama zilivyo Saund zao nyingine.
 
Wanayaonea wivu makampuni yanavyopata faida, hawajui makampuni yakipata faida kubwa ndo yanaweza kuongeza zaidi ubora wa huduma, kusambaza huduma, kupunguza bei ya huduma kwa mlaji na kuajiri watu wengi zaidi na hii inachochea ukuaji wa uchumi.

Nilisikitika sana Vodacom kulalamika kupata hasara ya bilioni 193 kutokana na serikali kuingiza tozo zake kwenye biashara yao ya M-PESA. Hawa watu wataua uchumi wa nchi kwa kuendekeza ubinafsi ili waendelee kununua magari ya kifahari ya V8 na wengine kuagiza mabasi ya Yutong..​
 
Mimi nitawaunga mkono iwapo watayabana haya Makampuni ya Simu yasituibie.

Nimeshuhudia Watanzania wengi wakituma sms pekee kuliko kupiga simu.

Maslahi ya mlaji yalindwe kisheria.
 
Hebu tuzitafakari hizi kauli mfu za Naibu Spika:

Ukizifikiria hizi kauli za Naibu Spika, utagundua ni kama serikali inaona gere kwa mapato wanayopata makampuni ya simu na mabenki kwenye miamala tunayoifanya wananchi.

Na ndiyo maana mara ya kwanza kabisa tozo zilipoletwa mwaka jana zilikuwa zinakaribiana sana na makato yale halali. Ukijumlisha na VAT wanayopata serikali basi ilikuwa ni kama tozo zinaendana sawasawa na makato ya muamala husika.

Hii thinking ya dunia ya ngapi? Kwamba kwa kuwa makampuni yanapata kikubwa kutoka kwa wananchi, basi ngoja tukapige mulemule na sisi tujipatie sawa sawa na wao bila kujali wanazidi kumkamua mwananchi?

Sasa kwa taarifa yake, siyo kwenye haya makato ya kidigitali tu, bali karibu sekta zote private entities ndizo zinapiga faida kubwa kuwazidi public entities. Na hiyo yote inasababishwa na wao wanasiasa, wanakuwa wanaingilia maamuzi ya professionals mwisho wa siku hao wataalamu wanaanza kufanya kazi kwa kuangalia upepo wa siasa unaelekea wapi na sio kitaalamu tena.

Wataalamu wetu wengi maofisini wamelishwa sumu ya u-ccm, yani maamuzi wanayofanya wanaangalia kwanza upepo wa siasa umekaaje. Nakumbuka sehemu moja nilihudhuria wakati wafanyakazi wapya wanafanyiwa induction, nilishangaa sana kumkuta mkurugenzi amekaa na ilani ya ccm mezani wakati huohuo hana kijaribu cha mission na visions za taasisi yake.

Mfano mdogo tuu, kwenye sekta ya afya hospitali binafsi ndizo zinapata pesa ndefu zaidi kutoka NHIF kushinda hospitali za umma. Mpaka juzi juzi NHIF wamelalamika kwamba eti kuna ujanja ujanja hawa private hospitals wanafanya, lakini ukweli ni kwamba hakuna ujanja wowote bali tuu inawauma privates kupata pesa nyingi kuzishinda public hospitals.

Sasa kwa akili kama hizi za wanasiasa wetu, tusitegemee kupiga hatua yoyote.

View attachment 2364333
nadhani imekuwa ngumu kidogo kujenga hoja zako vzr na kushindwa kufafanua kwa nn private hospitals zinapiga pesa nyingi.infact NHIF kwa kiasi hizi hospitali binafsi zina exaggerate matibabu.utakuta mgonjwa kaugua kihoma cha kawaida tu lkn anaandikiwa madawa kibao ambayo pia ni hatari kwa huyo mgonjwa.lakini nageukia kwa Ndugu Zungu,sidhani kama anauelewa wa maswala ya kodi sina uhakika.kama mabenki na makampuni ya simu yanapata faida kubwa hapa si inamaana hata serikali nayo inakamua pakubwa kupitia kodi?je mapato ya hayo makampuni yakipungua huoni hata serikali nayo itaathirika kimapato?labda mnisaidie wana JF mmemuelewa vzr naibu spika?mm kanichanganya kabisa.mbona wakati wananchi wanalalamikia kuhusu gharama za bando na kupiga simu wao walikuwa kimywa ndo leo wanaiona hiyo!hii nchi ni ngumu sana sijui hao watu wanafikiri kutumia nini.
 
Back
Top Bottom