Hebu tuzitafakari hizi kauli mfu za Naibu Spika:
Ukizifikiria hizi kauli za Naibu Spika, utagundua ni kama serikali inaona gere kwa mapato wanayopata makampuni ya simu na mabenki kwenye miamala tunayoifanya wananchi.
Na ndiyo maana mara ya kwanza kabisa tozo zilipoletwa mwaka jana zilikuwa zinakaribiana sana na makato yale halali. Ukijumlisha na VAT wanayopata serikali basi ilikuwa ni kama tozo zinaendana sawasawa na makato ya muamala husika.
Hii thinking ya dunia ya ngapi? Kwamba kwa kuwa makampuni yanapata kikubwa kutoka kwa wananchi, basi ngoja tukapige mulemule na sisi tujipatie sawa sawa na wao bila kujali wanazidi kumkamua mwananchi?
Sasa kwa taarifa yake, siyo kwenye haya makato ya kidigitali tu, bali karibu sekta zote private entities ndizo zinapiga faida kubwa kuwazidi public entities. Na hiyo yote inasababishwa na wao wanasiasa, wanakuwa wanaingilia maamuzi ya professionals mwisho wa siku hao wataalamu wanaanza kufanya kazi kwa kuangalia upepo wa siasa unaelekea wapi na sio kitaalamu tena.
Wataalamu wetu wengi maofisini wamelishwa sumu ya u-ccm, yani maamuzi wanayofanya wanaangalia kwanza upepo wa siasa umekaaje. Nakumbuka sehemu moja nilihudhuria wakati wafanyakazi wapya wanafanyiwa induction, nilishangaa sana kumkuta mkurugenzi amekaa na ilani ya ccm mezani wakati huohuo hana kijaribu cha mission na visions za taasisi yake.
Mfano mdogo tuu, kwenye sekta ya afya hospitali binafsi ndizo zinapata pesa ndefu zaidi kutoka NHIF kushinda hospitali za umma. Mpaka juzi juzi NHIF wamelalamika kwamba eti kuna ujanja ujanja hawa private hospitals wanafanya, lakini ukweli ni kwamba hakuna ujanja wowote bali tuu inawauma privates kupata pesa nyingi kuzishinda public hospitals.
Sasa kwa akili kama hizi za wanasiasa wetu, tusitegemee kupiga hatua yoyote.
View attachment 2364333