Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kifo cha Magufuli kimethibitisha pasipo shaka kuwa sisi kama nchi hatuna utaratibu wowote rasimi wa kikatiba, kisheria au usio wa kisheria unaotuongoza katika kuhesabu au kuzitambua awamu za serikali.
Kama utaratibu rasimi huo, basi ni wazi hauleweki na unapaswa kutazamwa upya ili kuondoa huu mkanganyiko unaojitokeza sasa tena ukiwahusisha viongozi wakubwa tu katika nchi yetu.
Hivyo, tunapaswa kuwa na utaratibu unaotamka rasimi kama awamu ya serikali inahesabiwa pale anapoingia Raisi mpya hata ikitokea Raisi aliepo madarakani anafariki na kurithiwa na makama wake au vinginevyo. .
Tujiulize, ikitokea tunapata Raisi mwingine kutokana na sababu zilizoainishwa na katiba yetu, Raisi huyo atakuwa ni wa serikali ya awamu ya tano, ya sita au ya saba?
Kwakuwa hatuna utaratibu unaoeleweka, hata awamu ya Nyerere inaweza isiwe ni awamu ya kwanza kwani zilikuwepo serikali za kikoloni kabla ya Nyerere kuwa Raisi.
Tujifunze kutokana na makosa kwa kuupatia suluhisho huu mkanganyiko uliopo sasa.
Kama ambavyo mikutano ya Bunge na vikao vyake viko well defined, basi na hizi awamu pamoja na chaguzi zake ziwe well defined.