Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

Ni suala la utashi tu hakuna mmiliki hata wewe unaeza ingia ukaiita awamu ya 6 na nusu

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni awamu ya Tano, tatizo walio kwenye mamlaka ndio wanaleta mkanganyiko..

Naamini hata katiba hii inaweza kutoa hilo suluhisho, kama ilisema Rais aliyeko madarakani akifa makamu wake anaendeleza kwa kuapishwa mbona hapo Katiba imeshamaliza....

Shida ni tafsiri tu hapo, na wahusika hawakuwa na muda na hilo....kifupi wanaosema hii ni awamu ta sita wanavunja katiba..

Salary slip unapaswa sasa kufungua kesi juu ya hili kuomba tafsiri...
 
Mi nakwammbia ngojea aje rais mwingine tutajua hatujui akijiita yeye ni awamu ya sita na waliopita ni awamu ya tano

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Leo bwashee umewaza vyema,kanywe mbege riverside nitalipa
 
Akuna cha awamu ya 6 hapa, ungeitishwa uchaguzi alafu atangaze serazake tuzipimei tuchague.
 
Unafahamu huu ni muhula kamili wa Rais aliyepo madarakani na hawezi kugombea zaidi ya muhula mmoja tena?
No. Amechukuwa awamu ya Magufuli anamalizia japo ni rais kamili. Tulifanya ''uchaguzi'' wa kutafuta serikali ya awamu ya tano, na ndiyo iliyoko bado madarakani. Awamu nyingine inaanza 2025.
 
Unafahamu huu ni muhula kamili wa Rais aliyepo madarakani na hawezi kugombea zaidi ya muhula mmoja tena?
kisiasa hii ni awamu ya 5, kwa kuwa ipo madarakani kwa kura za JPM (ndiye aliyechaguliwa kuwa Raisi, na Samia amekua raisi kwa kurithi).

kiutendaji, hii ni serikali iliyopo chini ya raisi wa 6 wa JMT..... naye ni Samia!

N.B; kiutendaj, mtu mwingine anaweza ku-argue kwamba hii ni serikali ya 7 ya tanganyika (kwa maana ya kuhesabu pia serikali ya Kawawa? aliyekua PM mara tu baada ya uhuru), so unakua na Kawawa, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia kwa sasa)........

ila kwa maana ya JMT basi hii kiutendaji na kiserikali ni serikali chini ya Raisi wa 6, awamu ya 5 ya utawala wa CCM nchini tanzania.

[emoji117]Awamu inakuja kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.

[emoji117]Serikali inaundwa kutegemea nani yupo madarakani muda huo, iwe ameingia kwa kurithi, kupindua au vinginevyo!
 
Kama awamu inakuja kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura hii ni zaidi ya awamu ya 10. Kwa sababu chaguzi zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka mitano tangu enzi za Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21.
 
Huu utaratibu wa “awamu” bila shaka tuliucopy kutoka nchi kama Marekani ambao wao wanakwenda na “rais wa X (37,38,40) hata kama Rais alitawala kwa mwaka mmoja tu.

Having said that, awamu in our case is meant to be namba ya Rais aliyepo. Mama Samia ni Rais wa 6 (soma awamu ya 6😊). Sijui kama hili lipo kwenye sheria au kanuni yoyote
 
Ni wazi hakuna kanuni wala sheria ya aina hiyo ndio maana tunatapata.
 
Kama awamu inakuja kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura hii ni zaidi ya awamu ya 10. Kwa sababu chaguzi zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka mitano tangu enzi za Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21.
kisiasa kuna awamu na vipindi, usichanganye....!

awamu ni neno letu la kisiasa likiwa na maana ya raisi aliyechaguliwa kwa kura!, vipindi vya utawala wake ni idadi ya mihula aliyogombea...!
 
Kama Raisi aliepo madarakani sasa aanaamini hii sio awamu ya tano bali ni ya sita, hauoni teyari huu ni mkanganyiko?

Tungekuwa na utaratibu maalumu au rasimi wa kikatiba, kisheria au vinginevyo unaotuongoza, haya yangetokea?

Samia ni Rais wa ngapi?
Na kuna jambo limewahi kukwama au kutokufanikiwa kwa ufanisi kutokana na matumizi ya neno " awamu"?

Samia ni Rais wa awamu ya sita.
 
Samia ni Rais wa ngapi?
Na kuna jambo limewahi kukwama au kutokufanikiwa kwa ufanisi kutokana na matumizi ya neno " awamu"?

Samia ni Rais wa awamu ya sita.
With reference to what?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…