Niko ukweni kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Hali ni mbaya. Umeme hakuna masaa 12 kwa siku. Yaani ni mwendo wa 0700 - 1900 kila siku.
Siku niliyofika nilidhani ilikuwa kutuwezesha nchi nzima japo kumwona Messi akichukua kombe baadaye usiku.
Kumbe hola!
Kumbe haya ndiyo maisha ya kanda ya ziwa wasikojua umuhimu wa kumweka Kipara kwenye vidole gumba kurudisha umeme kama tufanyavyo mjini?
Ninavyoandika hapa kama ada 0700 umeme umeshaliwa kichwa. Hii ni kama ilivyokuwa jana, juzi nk, tokea niingizane pande za huku.
Kulikoni wadau hali ikoje huko mliko nyie wenye kampuni lao wakiendelea kuchepusha maji Ruaha mkuu, kwa raha zao?
"Kwani nani atathubutu kuwagusa wajumbe wa bodi kihasara hasara? Kwani hajipendi yeye?" --in yoga's words.