Kumbe uniform moja ya staff wa atcl ni sh. 4.6 mil

Kumbe uniform moja ya staff wa atcl ni sh. 4.6 mil

Whisper

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2009
Posts
502
Reaction score
207
Kweli ukiwa na hasira unaweza ukapiga mtu risasi. Nimemsikiliza Mh. Mwakyembe akiongea na staff wa ATCL nikapandwa na hasira. Hii ni baada ya kulinganisha nilichokisikia kwenye Power Breakfast asubuhi ya leo na comments zilikonda za vilaza wa hicho kipindi. Mwanataaluma amekuja na facts ambazo kama ni Uchina tungekuwa tunauliza shimo la kutupia mizoga hiyo. Pamoja na utumbo mwingi walioufanya kwa kipindi hiki kifupi, Staff wawili wa ATCTL eti walikaa China mwezi mmoja na nusu kusimamia ushonwaji wa uniform 17 kwa gharama ya USD 49,900. Yaani ni wastani wa sh. 4.6 Mil kwa uniform. Sijajua zikoje..

Long live Dr. and stay blessed!! Sasa miezi ikisogea kimbia huko uje huku kwetu Peopleeeeeeeeez tumekuwekea nafasi.
 
Halafu kuna watu hapa wanasema Dr amewaonea wahusika...eti ni ukabila. Why have qwe become jokers? ATCL toka ubinafsishaji na baade kuchukuliwa tena na serikali ilichofanya ni nini zaidi ya ubadhilifu wa hela za walipa kodi? halafu wakiguswa wanasema ukabila, udini na maneno mengine mengi wanayoongea losers. Thanks, am not one of them,lol!
 
CHIZI NA WENZAKE WAMEKWAPUA usd 1m kwa tenda fake!pesa walilipwa na insurance company
 
Hakika Mwakyembe amenena leo, watanzania ni warahisi wa kutafuta sababu na miavuli ya kujifichia madhambi yetu mara dini au kabila. Ila kwa kweli Waziri amefanya maamuzi mazuri sana. Najaribu kufikiria kama hawajamaa wangekaa miaka 2 tena hili shirika lingeendelea kuwa ICU au kama siyo kufungwa kabisa.
 
Kama iko kwenye taarifa ya CAG tutaamini, lakini ukija na habari za kitoto kama hizi hakuna atakayeamini. Hakuna shirika wala kampuni katika dunia ya leo inayotuma mtu kwenda kushona nguo china. Pili kuna sheria ya manunuzi ya umma ambayo inaelekeza namna ya ununuzi. Msiwe wapumbavu wa kuamini kila kitu eti kwa vile amesema Mwakyembe, yeye sio CAG
 
Dr. Mwakyembe ulichofanya sio maamuzi magumu kama yanayosemwa na Ex- prime minister (Lowasa). Bali ni maamuzi SAHIHI kwa WAKATI MUAFAKA. Huu sio wakati watu kubebana. Ninachokuomba Dr. Mwakyembe nenda mguu na njia hadi Mamlaka ya Bandari utakuta madudu ama sio uchafu na ufisadi ulivyojaa. Nchi inakosa mapato kwa sababu ya watendaji wabovu na wabadhilifu.

Ni mimi,

Mpendamabadiliko
 
sasa imagine hao watu wa ATCL walioenda CHINA kushona yunifom wangekua ndio mawaziri wetu hali ingekuaje

ufisadi ni kila kona
 
Kama iko kwenye taarifa ya CAG tutaamini, lakini ukija na habari za kitoto kama hizi hakuna atakayeamini. Hakuna shirika wala kampuni katika dunia ya leo inayotuma mtu kwenda kushona nguo china. Pili kuna sheria ya manunuzi ya umma ambayo inaelekeza namna ya ununuzi. Msiwe wapumbavu wa kuamini kila kitu eti kwa vile amesema Mwakyembe, yeye sio CAG

Ndivyo demokrasia inavyoruhusu kuwa na maoni tofauti. Ila ili mtu awe kiongozi lazima awe na uwezo wa kutoa maamuzi magumu. Haya mambo yakusubiri mpaka 2015 kwenye kitu kinachoonekana kinaenda hovyo leo, wanafanya watu goigoi wasiohitajika tena kwenye hili Taifa. Kama mawaziri wote wakifanya kazi zao hivi watu wataacha kula hovyo mali ya umma. Imagine kwa mfano Ewura na TBS wameruhusu Agusta waingize mafuta mabovu toka ianze tender ya kuleta mafuta in bulk...nayo tumsubiri nani?
 
Kama iko kwenye taarifa ya CAG tutaamini, lakini ukija na habari za kitoto kama hizi hakuna atakayeamini. Hakuna shirika wala kampuni katika dunia ya leo inayotuma mtu kwenda kushona nguo china. Pili kuna sheria ya manunuzi ya umma ambayo inaelekeza namna ya ununuzi. Msiwe wapumbavu wa kuamini kila kitu eti kwa vile amesema Mwakyembe, yeye sio CAG

CAG anatuletea historia ya kile kilichotendeka zaidi ya mwaka moja au pengine miwili iliyopita. Wakati huo shirika litakuwa halina hata ndege moja lakini wafanyakazi wanendelea kulipwa na kodi za wananchi na watu wengine watakuwa wanalalama shirika lifufuliwe kwa vile ni la taifa. Napata kichefuchefu.

Kama aliyosema Mwakyembe ni uongo basi ATCL wakanushe siyo wewe isipoku wa kama una shahidi tueleze.

Nchi yetu imefilisika tunashindwa hata kushona magauni na skirt?
 
Mwenzenu hii nchi napata vidonda vya tumbo tu,tumekwisha kushnei babujii
 
Cha ajabu nini hapo wakati feniture za ikulu zinatoka china na wakati jkt wanachonga za ubao bora kabisa!
 
Kama iko kwenye taarifa ya CAG tutaamini, lakini ukija na habari za kitoto kama hizi hakuna atakayeamini. Hakuna shirika wala kampuni katika dunia ya leo inayotuma mtu kwenda kushona nguo china. Pili kuna sheria ya manunuzi ya umma ambayo inaelekeza namna ya ununuzi. Msiwe wapumbavu wa kuamini kila kitu eti kwa vile amesema Mwakyembe, yeye sio CAG

Watu wengine mnapenda sana kuharibu siku za watu.

Mwakyembe anawaambia ATCL staff kua sio poa nguo kushonewa China na wao hawabishi, anakuja mtu kwenye Keyboard ya simu au Computer uchwara na kudai Nguo hazijashonewa China, tena hajui hata hiyo Atcl iko wapi.

Huyo CAG wako usifikiri atatoa kila kitu, kwanza anakagua mashirika mangapi kwa mwaka??

Wala yeye sio mungu kiasi kwamba kama hajaona faulo basi haipo, hata "marudio ya kanda ya video" yanaweza kutumika kutoa maamuzi kama haikuonekana mwanzo.
 
Kumbe kuna uhusiano kati ya jina analopewa mtu na tabia zake...! Kwa sakata hili, nimeliamini hili....
 
Back
Top Bottom