"Niaje Wazeiyaaaah...
Mko Bwaxx....
Ebana katika majukum yetu haya ya ukandarasi nikajikuta (nikabahatika) majuz kufika USA.
Nisiwe na porojo sana, ni kwamba the way nilivokua napackia palivo, maisha na kila kitu ni tofauti kabisa na nilivokuta.
yan hakuna toafuti na bongo.
Cku ya kwanza tu nafika nikashangaa mbona watu weusi ndio wengi huku???
Mbona wanaongea Kiswahili kama bongo tuu??
kama haitoshi hadi fedha wanayotumia ni Tanzanian Shillings.
Sio hivo tu, hadi bangi, mateja na miziki inayopigwa kwa radio statios na night clubs ni kama bongo tuuu
Yaani kifupi USA hakuna tofauti na bongo.
Kidoogo labda ka ubaridi kule kamezidi.
Sasa KILICHONIACHA HOI kabisa mpaka nikaamua kutype haya maneno ni kuwa:
Mpaka bank ya NMB ina tawi lake liko USA bana huwez amini.
Mimi nilidhani "USA River" ni pakishuua kumbe kama bongo Dar es salaam tuu."
Umenikosha mkuu